Ruto ameteua wasimamizi wa kampeni za 2027-Mbadi azungumzia uteuzi wa mawaziri

"Baraza la mawaziri lina upungufu wa sifa za kitaaluma, uwezo wa kitaaluma, uzoefu na uadilifu."

Muhtasari
  • Akizungumza Jumatano, Mbadi alidai walioteuliwa  mawaziri watakuwa wasimamizi wa kampeni za Ruto
Kiongozi wa wachache John Mbadi akionyesha kidole chake baada ya kuzozana na Mbunge wa Sigowet/Soin Kipsemgeret Koros
Kiongozi wa wachache John Mbadi akionyesha kidole chake baada ya kuzozana na Mbunge wa Sigowet/Soin Kipsemgeret Koros
Image: LUKE AWICH

Mbunge wa Suba Kusini John Mbadi amesema kuwa Rais William Ruto yuko tayari kuendesha serikali kutoka Ikulu kwa kutumia washauri wala si Makatibu wa Baraza la Mawaziri.

Akizungumza Jumatano, Mbadi alidai walioteuliwa  mawaziri watakuwa wasimamizi wa kampeni za Ruto.

“Ni kweli Rais ameteua wasimamizi wa kampeni za 2027. Rais anatuambia tu tumpe baraza la mawaziri ambalo halitafanya kazi kwa sababu yuko tayari kuendesha serikali yote kutoka Ikulu kwa kutumia washauri,” alisema.

"Baraza la mawaziri lina upungufu wa sifa za kitaaluma, uwezo wa kitaaluma, uzoefu na uadilifu."

Aliongeza kuwa wengi wa walioteuliwa wameshtakiwa kwa kesi za ufisadi.

Bunge liliidhinisha kwa kauli moja wateule wote wa baraza la mawaziri waliopendekezwa na Rais William Ruto.

Wabunge hao waliwaondoa walio wachache ambao wameibua masuala kuhusu uadilifu na taaluma ya mteule wa Utumishi wa Umma Aisha Jumwa na mwenzake wa Kilimo Mithika Linturi.