Davido alazimika kuifuta akaunti ya Instagram ya marehemu mwanawe

Hatua hii inatokea wiki moja tu baada ya taarifa kusambaa kuwa mtoto huyo wake alizama kwenye bwawa la kuogelea nyumbani.

Muhtasari

• Ikumbukwe akaunti hiyo ya kijana huyo ilifunguliwa mapema mwezi jana wakati walikuwa wanamsherehekea kufikisha umri wa miaka mitatu.

Davido aifuta akaunti ya Instagram ya mwanawe
Davido aifuta akaunti ya Instagram ya mwanawe
Image: Instagram

Mwanafalsafa mmoja aliwahi sema kwamba hakuna kitu cha kufadhaisha moyo na kuuma mno kuliko jino kama kulazimika kufuta namba ya mtu wako wa karibu kutoka kwa simu yako, si kwa sababu mmekosana, bali kwa sababu hayupo duniani tena!

Kauli kama hii inatafsiriwa vizuri na kile ambacho familia ya mwanamuziki kutoka Nigeria Davido na mkewe Chioma wanapitia kipindi hiki kigumu baada ya kumpoteza mwanao, Ifeanyi mwenye umri wa miaka 3.

Familia hiyo ya kistaa ilikuwa imemfungulia akaunti ya Instagram mwanao, akaunti ambayo ilikuwa imekua kwa kasi za duma na mpaka kifo chake tayari ilikuwa na wafuasi zaidi la elfu 50.

Baada ya kifo chake, wanandoa hao kwa uchungu mwingi wamelazimika kuifuta akaunti hiyo na kufuta picha zake zote, kama moja ya njia ya kujaribu kudhibiti jinsi watu wanasambaza picha za marehemu kijana wao, na pia kujaribu kupata faraja.

Ikumbukwe akaunti hiyo ya kijana huyo ilifunguliwa mapema mwezi jana wakati walikuwa wanamsherehekea kufikisha umri wa miaka mitatu ambapo baba yake alimuandikia ujumbe mzuri wa kumtabiria kuwa mkubwa zaidi kimafanikio kumliko – lakini kwa bahati mbaya kifo kikakatisha ndoto yake pamoja na ya wazazi wake.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu mrithi wa nyota huyo wa muziki wa Nigeria anasemekana kuzama kwenye bwawa la kuogelea nyumbani kwao Lagos. Maelezo yanaonyesha kuwa Davido na Chioma walikuwa mbali katika Jimbo la Ibadan kwa ajili ya mkusanyiko wa familia ajali hiyo ilipotokea. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, kijana huyo alipatikana akiwa amepoteza fahamu kwenye bwawa la kuogelea na kukimbizwa katika hospitali ya Lagos, ambapo alitangazwa kuwa amefariki