Nitaunga mkono pendekezo la kuondoa muhula wa rais-Cherargei

Cherargei aliongeza kuwa mbunge wa Fafi Salah Yakub aliyetoa pendekezo hilo ana haki ya kushinikiza marekebisho hayo.

Muhtasari
  • “Chama cha UDA kinazingatia demokrasia na utawala wa sheria. Mheshimiwa Salah Yakub ana haki ya kushinikiza marekebisho hayo
Star, KWA HISANI
Star, KWA HISANI
Image: Samson Cherargei

Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei amesema ataunga mkono pendekezo la kuondoa muhula wa kuhudumu wa rais iwapo litawasilishwa katika bunge la Seneti.

Kupitia mtandao wake wa Twitter Jumatano, Cherargei aliongeza kuwa mbunge wa Fafi Salah Yakub aliyetoa pendekezo hilo ana haki ya kushinikiza marekebisho hayo.

“Chama cha UDA kinazingatia demokrasia na utawala wa sheria. Mheshimiwa Salah Yakub ana haki ya kushinikiza marekebisho hayo, ni vyema tumsikilize kwanza, nitaunga mkono pendekezo hilo katika bunge la Seneti. Hili ni swala ambalo linaweza likajadiliwa siku za usoni,” alisema Seneta Cherargei.

Pendekezo la mbunge huyo wa chama cha  UDA limeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya na pia katika ulingo wa kisiasa.

Hata hivyo cham hicho kilikana madai hayo siku ya Jumanne, kupitia kwa mwenyekiti wao Muthama

Mbunge Yakub alisema kuwa atawasilisha mswada bungeni ili kuona kwamba kipengele hicho kinafutiliwa mbali na badala yake kubadilishwa na kipengele cha umri wa rais atakayekuwa akihudumu madarakani.