Mwanaume njia panda kwa kutakiwa kutimiza masharti mengi kumuoa mpenziwe Mkamba

Ngo'mbe 84, mbuzi 12, matenki 3 ya maji, fimbo ya mzee inayogharimu laki moja ni miongoni mwa masharti maumu aliyopewa.

Muhtasari

• Alitakiwa kuleta mitungo minne ya ndizi mbichi pamoja na mitungi 10 ya lita ishirini ikiwa imejazwa na mvinyo wa kiasili.

• Kando na hayo, alitakiwa kutoa debe 2 za asali ya kiasili pamoja na kabuti ya mzee inayogharimu nusu laki mionhoni mwa vitu vingine vingi.

Image: twitter

Mwanamume Mkenya kwa jina Heyi Gregory ameachwa kinywa wazi baada ya kukabidhiwa orodha ya mahitaji ya mahari kwa ajili ya kumuoa mpenzi wakekutoka jamii ya Akamba. Wanamitandao wa Twitter walioona orordha hiyo walikisia kwamba gharama hiyo ya mahari ni ghali mno ya kutosha pengine kujenga nyumba ya vyumba viwili!

Mwanamume huyo alifichua picha ya matakwa yote aliyoorodheshewa kutimiza na kwenye Twitter alipakia picha hiyo na kuifuatisha kwa mada 'malipo ya sherehe ya mahari ya kitamaduni ya Kamba'.

Aliwaulizia wanamitandao katika kile kilionekana kuwa alikuwa akitaka kubaini ikiwa ndivyo harusi ya kitamaduni ya waKamba inavyodai au ilibadilishwa ili kujumuisha masilahi ya kibinafsi kutoka kwa upande wa bi harusi.

Kwa sherehe za kufundwa orodha hiyo ilijumuisha mbuzi watano, kreti mbili za bia, lita 40 za bia ya kienyeji, blanketi nne za kiwango cha sita na mashuka kila moja, kreti mbili za ndizi mbivu na kreti tatu za soda.

Kana kwamba hiyo haitoshi, orodha tofauti ya malipo ya mahari pia iliwasilishwa. Bidhaa ya kwanza kwenye orodha ilikuwa mbuzi 84, ng’ombe 12, matangi matatu ya maji ya lita 10,000, kreti nane za bia, madumu kumi ya lita 20 za bia ya kienyeji na vipande 4 vya ndizi mbichi.

Ili kumpatia jasho zaidi, familia hiyo pia iliomba debe 2 za asali au kilo 100 za sukari, seti 12 za mashina 12 ya miwa, magunia manne ya kilo 90 ya mahindi. na kilo 90 za maharage, 'fimbo ya mzee' kwa gharama ya Sh 100,000, 'kabati' yake Sh 50,000; na kitu kikingine kwa jina nduua itaa kwa jumla ya gharama ya Sh 50,000, Mukwa kwa shilingi 300,000.

Picha ya matakwa hayo mengi yenye bei ghali ilizua mjadala mkali kwa takribani wikendi nzima huku baadhi wakimshauri kuenda mbele na kutii matakwa yote huku wengine wakimshauri kuzima taa kabisa na kusahau mpenzi huyo wake.

Je, wewe ungemshauri afanyeje? Na vipi kama ungekuwa wewe?