Robert Alai amkosoa gavana Nyong'o kwa kukashfu uteuzi wa mawaziri wa Ruto

Badala yake, Alai alimtaka gavana Nyong'o kushirikiana na rais ili kuleta maendeleo katika kaunti ya Kisumu.

Muhtasari

• Alimtaka kuwaachia malalamiko kama hayo watu wa nyadhifa za chini kama maseneta, wabunge na hata madiwani.

Alai amkosoa Nyong'o kwa kunyooshea kidole uteuzi wa mawaziri wa Ruto.
Alai amkosoa Nyong'o kwa kunyooshea kidole uteuzi wa mawaziri wa Ruto.
Image: Facebook

Diwani wa Kileleshwa amabye pia ni mwanablogu Robert Alai amemkosoa vikali gavana wa Kisumu profesa Anyang’ Nyong’o baada ya kuchangia Makala ya kumkashfu rais Ruto kwenye moja ya magazeti ya humu nchini.

Katika Makala hayo, Nyong’o alitoa maoni yake katika Makala ndefu akielezea mfadhaiko wake kuhusu jinsi rais Ruto alifanya uteuzi wa baraza lake la mawaziri.

Gavana huyo anayehudumu kipindi chake cha pili kama rais wa kaunti ya Kisumu alisema kuwa Ruto alikosea vikali mno kutoonesha muunganiko wa kitaifa katika kuteua mawaziri wake.

“Sasa, marafiki zangu, wakati nafasi nyingi za Baraza la Mawaziri na Katibu Mkuu zinapogawanywa kati ya maeneo ya Kati ya Kenya na Bonde la Ufa, je, sisi wengine tunawezaje kuhukumu tafsiri ya Rais kuhusu maana ya "usawa"?” Nyong’o aliuliza.

“Tunachoshuhudia sasa ni dhahiri si siasa za utangamano wa kitaifa au umoja, bali ni ukabila, unaoitwa ukabila.”

Alizidi kuitetea kauli yake kwa kusema kuwa yeye kama mkenya yeyote yule ana haki na uhuru wa kumkosoa rais anapoenda kinyume na matarajio ya wananchi walipa ushuru.

Baada ya kutoa kauli hii, Alai alionekana kutokubaliana naye na kupitia ukurasa wa Facebook wa gavana Nyong’o alikokuwa amepakia ‘link’ ya kuelekeza wasomaji kwenye makali hayo yake, Alai alimkosoa.

Kulingana na Alai, gavana Nyong’o amepitia kutoa maoni kama haya na badala yake anafaa kujikita katika kuleta maendeleo katika kaunti ya Kisumu kwa kushirikiana na rais Ruto.

Alimtaka kuwaachia malalamiko kama hayo watu wa nyadhifa za chini kama maseneta, wabunge na hata madiwani.

“Wewe ni kiongozi mkuu wa kaunti. Kampeni hizi waachie Wabunge, Maseneta na MCAs. Shirikiana na Rais kujenga kaunti yetu,” Alai alimshauri profesa Nyong’o.