Ruto na Gachagua hulala 2am na kurauka 4am - Mbunge wa Soy, David Kiplagat

Alisema kuwa viongozi hao wanahangaika usiku na mchana ili kunyoosha mambo kwa faida ya Wakenya.

Muhtasari

• Naweza kukuambia kuwa rais, naibu wake, na Baraza lao la Mawaziri huamka saa kumi asubuhi na kulala saa nane asubuhi kwa ajili ya kufanya kazi kwa nchi hii - Kiplagat.

Mbunge wa Soy awatetea Ruto na Gachagua
Mbunge wa Soy awatetea Ruto na Gachagua
Image: Maktaba, screengrab

Ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu Kenya ipate serikali mpya inayoongozwa na rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua.

Licha ya viongozi hao kuahidi kupunguzia Wakenya mzigo mzito wa kiuchumi na gharama ya juu ya maisha, bado wakenya wengi wangali wanahisi bado serikali mpya haijapata sduluhu kwani kuteseka kumekuwa kama sehemu ya maisha ya kila siku.

Mbunge wa Soy, David Kiplagat sasa anamtetea rais Ruto na naibu wake Gachagua kwa kile anasema kuwa viongozi hao wawili tangu kuapishwa rasmi hawajawahi kupata usingizi wa kutosha.

Kiplagat ambaye alikuwa anazungumza katika mahojiano na runinga moja ya humu nchini, alisema kuwa Ruto na Gachagua wamekuwa wakirauka alfajiri ya saa kumi na kuingia kitandani saa nane usiku kutokana na mihangaiko ya kujaribu kutafuta suluhu la matataizo yanayowasabahi wakenya kila kona.

“Naweza kukuambia kuwa rais, naibu wake, na Baraza lao la Mawaziri huamka saa kumi asubuhi na kulala saa nane asubuhi kwa ajili ya kufanya kazi kwa nchi hii. Kwa hiyo, tunafanya kazi; Haupaswi kuzingatia kile kinachotokea katika mkutano wa hadhara au mkusanyiko kana kwamba hapo ndipo sera zinaundwa. Sera zinafanywa katika ofisi na vyumba vya mikutano,” Kiplagat alifichua.

Mbunge huyo amabye ni mwandani wa rais Ruto alisisitiza kwamba kwa miezi miwili ambayo serikali ya Kenya Kwanza imekuwa uongozini, wamefanikiwa kufanya asilimia 98 ya kazi kwa Wakenya na kuahidi kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu madeni mengi kwa kampuni ya Uchina ya kutengeneza barabara mayakuwa yamelipwa kikamilifu.

“Wachina wanaposaini mikataba wanasaini miwili mmoja wa mkataba halisi na mwingine wa refinancing na kila mara wanapata refinancing kupitia benki ya Exim ndio maana wanaweza kuendelea na miradi yao japokuwa wakati mwingine serikali inakosa fedha, ni jambo ambalo wakandarasi wetu wa ndani wanapaswa kuzingatia," alieleza