Samahani-Aisha Jumwa aomba radhi baada ya kumtambua Rais Ruto kama 'Naibu Rais'

"Mimi nataka nichukue nafasi hii kwanza kabisa nimshukuru Naibu wa...," alinyamaza huku wananchi wakiangua kicheko

Muhtasari
  • Jumwa hakuwa mwepesi kuomba msamaha akisema kuteleza kwake ulimi ni kwa sababu alizoea kumwita Ruto, Naibu Rais kwa muda mrefu
Image: FACEBOOK// AISHA JUMWA

Kulikuwa na nyakati za kufurahisha wakati wa hafla ya kuzindua kiwanda cha Devki Steel Mills, kiwanda hicho kilizindduliwa na Rais William Ruto siku ya Ijumaa.

Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Utumishi wa Umma na Jinsia Aisha Jumwa aliwaacha watazamaji wakiwa wameduwaa baada ya kumtambua Ruto kama Naibu Rais.

"Mimi nataka nichukue nafasi hii kwanza kabisa nimshukuru Naibu wa...," alinyamaza huku wananchi wakiangua kicheko

Baada ya matamshi yake Jumwa Rais Pia alionekana akiangua kicheko.

Jumwa hakuwa mwepesi kuomba msamaha akisema kuteleza kwake ulimi ni kwa sababu alizoea kumwita Ruto, Naibu Rais kwa muda mrefu.

"Samahani, kunradhi, tumeishi naye kama naibu wa rais sana," alisema.

Alimshukuru Ruto kwa kumpa nafasi ya kuhudumu katika Baraza la Mawaziri.

"Ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru rais kwa kunichagua kuwa waziri katika Baraza la Mawaziri," alisema.

Ni heshima kubwa kuwa amewapa wananchi wa Pwani fursa, ingawa mimi si waziri wa pwani, mimi ni waziri wa Kenya, nilipochukua kiapo nilichoapa kuwa Waziri Mkuu wa nchi nzima."