Mwanaume amfumania mkewe mjamzito akila uroda na mchungaji ndani ya chumba chake

Mwanaume huyo aliondoka kwenda safarini ila njiani akabadili mawazo na kurudi nyumbani ghafla alipowafumania wawili hao kitandani mwake.

Muhtasari

• Si tu aliwafumania wakishiriki tendo la ndoa bali pia alipata vitu vinavyoaminika kuwa vya kishirikina vimetapakaa ndani mwa chumba chake

Image: MAKTABA

Kwenye mtandao wa Twitter, kuna video ambayo imekuwa ikisambazwa ya mwanaume mmoja ambaye alimfumani mkewe mjamzito akiwa anakula uroda na mwanaume mwingine katika kitanda chao cha ndoa.

Tukio hilo linaloaminika kutokea nchini Zambia linaonesha mwanaume mwenye nyumba akiingia katika chumba chao cha kulala na kwa mshangao mkubwa anamfumania mkewe mwenye ujauzito mkubwa akiwa uchi wa mnyama kitandani na mwanaume mwingine ambaye alikuwa anajiita mchungaji wa kanisa.

Mwanamke huyo, aliyejulikana tu kama Martha, alikuwa amemwambia mumewe kuwa alikuwa anaodnoka kwa ajili ya kuitembelea familia yake huko Kitwe nchini Zambia. Mumewe baada ya kumuaga aliondoka lakini ufika njiani alibadili mawazo na kurudi ambapo alipigwa na butwaa kile alichokiona kikitendeka chumbani mwake.

Si tu aliwafumania wakishiriki tendo la ndoa bali pia alipata vitu vinavyoaminika kuwa vya kishirikina vimetapakaa ndani mwa chumba chake cha malazi huku wawili hao wakiwa uchi.

Video iliyorekodiwa na mume huyo ambayo imesambaa mitandaoni, inaonyesha mume akimwambia mke huyu asisogee, kwamba atamuua.

Mke akiwa bado uchi alijaribu kumsihi mumewe, huku mchungaji akishindwa kujikwamua na kuharakisha kuvaa kaptula yake ili kuficha uchi wake.

Tukio hilo lilikuwa la kustaajabisha kwani mchungaji aliyetajwa, ili kuogofya kivuli cha mume wa Martha au kufanya chumba kuwa cha kimapenzi alikuwa amepamba chumba kwa mishumaa, maua na vitu vingine vilivyokuwa sakafuni.

“Usisogee. Nitakuua. Usisogee. Usitembee,. Shuka!!! Juu ya kitanda changu, Martha… Juu ya kitanda changu, Martha. Uliniambia unaenda Kitwe…. Hii ni nini??!!...Usinikaribie! … Vipi kuhusu haya yote katika nyumba yangu? Vipi kuhusu haya yote nyumbani kwangu?” Lakini mwanamke huyo, alionekana kuinama chini ili kuficha uso wake kutoka kwa kamera huku akijifanya kulia kwa kujuta.

Video hiyo hatuwezi kuichapisha hapa kutokana na sababu za kimaadili!