Wafungwa walijaribu kunilawiti gerezani - msanii Majirani afunguka

Mimi ni mjuzi mzuri sana wa maswala ya Taekwondo na hilo lilinisaidia sana - Majirani.

Muhtasari

• Alisema babake alimpeleka kituoni kama kumwadhibu lakini alipowapiga walawiti akajizolea kibano cha miezi 11 jela.

Majirani asimulia kidogo kulawitiwa
Majirani asimulia kidogo kulawitiwa
Image: Facebook//Majirani

‘Hivo ndio kunaendanga!’ bila shaka kwa wapenzi wa muziki wa Kenya wakisikia mstari huo kitu kinapiga kichwani ni kundi la wasanii wa lebo ya Grandpa enzi hizo likijumuisha Majirani, Kenrezy na Visita.

Wasanii hao waliteka anga ya muziki wa Kenya mapema kati ya mwaka 2010 na 2019 kabla ya kutoweka na kila mmoja kujishughulisha na biashara yake.

Msanii Majirani ambaye alifanya wimbo huo na kuwashirikisha wenzake hao wawili alipata kufanya mahojiano na kipekee na Nairobi News na kuzungumzia mambo ya ajabu ambayo aliwahi kuyapitia maishani mwake.

Majirani alielezea kwamba babake alikuwa anamlazimisha kufanya kitu ambacho yeye moyo wake haukuwa unakitaka kwa vile yeye alikuwa na msukumo wa ndani kwa ndani kufanya muziki.

Kutokana na kupishana na babake kimaneno, ilimpelekea kukwaruzana kidogo na mzee wake akaamua kumpeleka jela kama njia moja ya kulainika na kupata adabu.

“Unajua katika maisha lazima ufuate kitu amnacho moyo wako unataka. Sikuchagua kosi hiyo,babangu alinichagulia lakini mimi nilikuwa nataka kufanya muziki. Na hiyo ndio sababu nilikuwa na mkwaruzano na babangu hadi akaniweka jela kama njia ya kuniadhibu,” Majirani alieleza jinsi alijipata nyuma ya nondo kwa mara ya kwanza maishani mwake.

Akiwa jela, mambo yasiyofurahisha yalimtokea ambapo baadhi ya wafungwa wakongwe walijaribu kumlawiti ila njama yao ikafeli.

Msanii huyo kwenye mahojiano alieleza kwamba alipambana nao kiume kwa kukataa kulawitiwa na katika makabiliano hayo akawaumiza, jambo lililozidisha kifungo chake gerezani hata zaidi.

“Wakati nilikuwa hapo ndani, kitu kibaya fulani kikanitokea. Kuna vijana wanaota maordinary walinivamia mule ndani, mimi ni mwathirika wa kulawitiwa. Walijaribu kunilawiti kwa fujo lakini ilinibidi nipiganie maisha yangu. Mimi ni mjuzi mzuri sana wa maswala ya Taekwondo na hilo lilinisaidia sana. Kwa hiyo katika ile hali ya kujitetea nisilawitiwe, baadhi yao walipoteza meno na hilo lilinisababishia kufungwa jela miezi 11,” Majirani alibua kumbukumbu mbaya.