Mbunge wa ODM awakejeli wakulima wa bonde la ufa kuhusu mahindi ya GMO

Haya yanajiri baada ya video ya zamani ya Mhe Raila Odinga akiunga mkono GMO kuibuka mitandaoni.

Muhtasari
  • Ni hatua ambayo imechukuliwa baada ya seneta wa Nandi Cherargei Samson kusema kuwa serikali haifai kuagiza mahindi kutoka nje kwa kuwa wakulima wako katika kipindi cha kuvuna
PETER KALUMA
Image: HISANI

Mbunge wa Orange Democratic Movement Mhe. George Peter Kaluma amewakejeli wakulima wa Bonde la Ufa kuhusu mahindi ya GMO ambayo yalitarajiwa kuagizwa nchini hivi majuzi baada ya Waziri wa Biashara Mhe Moses Kuria kudaiwa kutangaza.

Kulingana na Mhe Kaluma kwenye matamshi yake kwenye akaunti yake ya twitter amesema kuwa Kaskazini na Kusini mwa Rift haipaswi kufikiria kulima mahindi kwani GMO tayari iko hapa na kwamba uhuru umefika.

"Wacheni ukulima wa mahindi Kaskazini na kusini mwa rift Uhuru umekuja,"Kaluma alisema.

Haya yanajiri baada ya video ya zamani ya Mhe Raila Odinga akiunga mkono GMO kuibuka mitandaoni.

Wakati huo huo leo, katibu wa baraza la mawaziri wa biashara Moses Kuria amesema kuwa serikali haitaagiza tena mahindi ya GMO kwa vile wanatazamiwa kuagiza mahindi bila malipo nchini ndani ya miezi sita wanapofanyia kazi mahindi ambayo tayari yamevunwa huko Rift.

Ni hatua ambayo imechukuliwa baada ya seneta wa Nandi Cherargei Samson kusema kuwa serikali haifai kuagiza mahindi kutoka nje kwa kuwa wakulima wako katika kipindi cha kuvuna.