'Muungano wa Azimio ulisimama na wewe,'Ledama amzima Kanini Kega baada ya madai ya kusalitiwa

Kanini akizungumza siku ya Jumatano alisema kwamba alishtuka sana wakati wa kupigia wabunge wa EALA kura

Muhtasari
  • Ledama alimsfahamisha Kanini kwamba muungano huo ulisimama naye na hata alimpigia kura, na kusimama naye badala ya kusimama na Kioni
LEDAMA 2
LEDAMA 2

Seneta wa Narok Ledama Ole Kina kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amemjibu mbunge mteule wa EALA Kanini Kega, baada ya madai yake kwamba alisalitiwa.

Kanini akizungumza siku ya Jumatano alisema kwamba alishtuka sana wakati wa kupigia wabunge wa EALA kura kwani wabunge kutoka mrengo wa Azimio waliwapigia watu asiowajua licha yakee kusimama na muungano huo.

Ledama alimsfahamisha Kanini kwamba muungano huo ulisimama naye na hata alimpigia kura, na kusimama naye badala ya kusimama na Kioni.

"Rafiki yangu @Kaninikega1 muungano wa azimio ulisimama na wewe, nilikupigia debe na nikakupigia kura ndio maana ulishinda, ukweli ni kuwa tulikuchagua badala ya @HonKioni,"Ledama alisema.

Kanini alisema Gachagua ameweka kazi ya kuunganisha eneo la Mlima Kenya jambo la kupongezwa.

"Gachagua alifanya vyema katika kuunganisha eneo la Mlima Kenya. Ni kiongozi mkuu pekee tuliye naye. Tunahitaji kuungana naye kama kanda," alisema.

"Ninataka kumshukuru Gachagua ambaye aliona kuwa eneo la Mlima Kenya litakuwa na tatizo ikiwa hatutawakilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki."