Naona watu wakiimba yote yawezekana hivi karibuni-Ledama Olekina asema

Ametabiri kuwa kutokana na sababu hiyo haitashangaza iwapo wataanza kuimba wimbo maarufu wa yote yawezakana

Muhtasari
  • Inavyoonekana amewasuta Wakenya na KKA ya Ruto kwa kukumbatia mpango wa kuhalalisha mahindi ya GMO

Seneta mashuhuri wa Narok na mfuasi mkuu wa Azimio la Umoja one Coalition Hon Ledama Olekina amesema kwamba yeye sio nabii lakini anaona  mambo yanavyoenda wakenya wataanza kuimba kibao cha yote yawezekana,

Inavyoonekana amewasuta Wakenya na KKA ya Ruto kwa kukumbatia mpango wa kuhalalisha mahindi ya GMO.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter, Ledama Olekina amefichua chuki yake kubwa kuhusu mpango wa hivi majuzi wa serikali wa madai ya kuongeza karo za shule Januari.

Aidha seneta huyo  ameshambulia serikali  kwa kuingiza vyakula vya GMO nchini ili kutokomeza makali ya njaa

Kulingana naye, licha ya mabishano hayo yote, Wakenya hawaonekani kuwa na wasiwasi na kuna uwezekano wanafumbwa macho na KKA.

Ametabiri kuwa kutokana na sababu hiyo haitashangaza iwapo wataanza kuimba wimbo maarufu wa yote yawezakana hivi karibuni ili tu kuishangilia serikali.

Sambamba na hilo, Ledama ameonya kuwa Wakenya wajiandae kukabiliana na hali ngumu mbeleni kwani serikali wanayokumbatia itawalazimisha kulipa ada maradufu kabla ya Januari.

Pia amefahamisha kuwa licha ya vyakula vya GMO kuwa na athari chanya, pia vina madhara yake na Wakenya wanapaswa kuwa na wasiwasi.

"Are you guys serious? Kuanzia Januari ada ya shule itaongezeka maradufu, vyakula vya GMO vitakuwepo na madhara makubwa kama vile kupungua kwa hamu ya kula na bado unasema Kenyan Kwanza? Mimi sio nabii lakini naona watu wakiimba wimbo maarufu 🎵🎶 Yote yawezekana hivi karibuni katika mitaa ya nairobi."