Mama afariki 'kutokana na huzuni' siku 3 baada ya kugundua kifo cha mwanawe

Kifo chake kilihusishwa na huzuni aliokuwa amejawa nao baada ya kuarifiwa kuwa mwanawe mwenye umri wa miaka 34 alikuwa amefariki.

Muhtasari

• Elizabeth Ilich alifariki siku tatu baada ya kuupata mwili wa mwanawe Goran Ilich mwenye umri wa miaka 34.

Mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu
Image: Instagram//Azam

Mwanamke mmoja aliripotiwa kufa kutokana na huzuni na simanzi baada ya kugundua kuwa mtoto wake alifariki – mwanamke huyo alikufa siku tatu baadae baada ya kuomboleza mfululizo.

Jarida la Daily Mail liliripoti kwamba mwanamke huyo, Elizabeth Ilich alifariki siku tatu baada ya kuupata mwili wa mwanawe Goran Ilich mwenye umri wa miaka 34.

“Siku tatu baada ya kifo chake, mamake Goran aliaga dunia katika kile ambacho wenyeji walikiita 'msiba wa kufuatana'. Mapema asubuhi ya Jumatatu, Elizabeth Ilich aliyejawa na huzuni aliamka akiwa na maumivu ya kifua na kuwaita marafiki kwa usaidizi. Ambulensi iliitwa lakini Bi Ilich aliaga dunia katika hospitali saa chache baadaye. Marafiki wamesimulia kwamba Bi Ilich alikuwa na ugonjwa wa moyo na wanaamini kuwa huzuni ya kifo cha mwanawe ilisababisha mshtuko wa moyo,” Daily Mail waliripoti.

Tukio hili liliripotiwa na majarida mengi ya kimataifa kama moja ya matukio nadra sana kushuhudiwa kwa binadamu kufa kutokana na huzuni wa kumpoteza mpendwa wao.

Nchini Kenya wiki kadhaa zilizopita msiba sawia na huyo uliigubika familia ya mbunge wa Chuka Igambang’ombe Patrick Munene ambaye alipoteza binti wake na babake katika wiki moja.

Babake Munene aliaga dunia siku ya Jumanne, Novemba 1, 2022, huku bintiye akiaga dunia siku ya Jumamosi, 5, 2022. Munene alikuwa akijiandaa kwa maziko ya babake wakati habari kuhusu binti yake zilipokuja.