Siku moja utakuwa naibu wangu-Babu Owino amwambia Charlene Ruto

"Charlene Ruto unafanya kazi nzuri. siku moja utakuwa naibu wangu,"Babu Aliandika.

Muhtasari
  • Charlene Ruto amekuwa akifanya kazi kupita kiasi hivi majuzi huku wengi wakihoji hatua zake za hivi majuzi
Mbunge wa Embakasi East Babu Owino
Image: Facebook// Babu Owino

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino alitoa maoni na kumsifu bintiye Rais Ruto kwa kazi nzuri anayofanya.

Kwenye chapisho lililotolewa na Charlene Ruto leo ambapo aliomba kuambiwa jambo na wafuasi wake,Babu Owino alimwambia kwamba anaffanya kazi nzuri na siku moja atakuwa naibu wake.

Babu hakuweka wazi ni naibu wa nini au cheo kipi.

"Charlene Ruto unafanya kazi nzuri. siku moja utakuwa naibu wangu,"Babu Aliandika.

Charlene alijibu na kuthamini maoni hayo.

"ASante Babu Owino."

Charlene Ruto amekuwa akifanya kazi kupita kiasi hivi majuzi huku wengi wakihoji hatua zake za hivi majuzi.

Ameonekana akiwa na viongozi mbalimbali nchini Kenya na nje ya Kenya.

Alikuwa katika kaunti ya Narok leo na siku zilizopita alionekana Bomet, Kisii na Nairobi. Pia amekuwa akiwashirikisha vijana na kutembelea takriban kaunti zote nchini.

Mashabiki nao waliungana kumuunga mkono kwa kazi nzuri anayoifanya ingawa bado haijawekwa wazi nafasi anayoshikilia serikalini.