Kifo cha Chiloba ni hasara kubwa kwa jamii,'Passaris asema huku akiishukuru serikali ya Marekani

Haya yanajiri baada ya serikali ya Marekani pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kulaani mauaji ya kikatili

Muhtasari
  • Passaris aliongeza kwamba tunapaswa kuunda jamii inayojumuisha wote ambapo kila mtu anakubalika na pia kutibiwa kwa usawa
Mwanaharakati wa LGBTQ, Chiloba
Mwanaharakati wa LGBTQ, Chiloba
Image: Instagram

Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Nairobi Esther Passaris amejitokeza na kuishukuru serikali ya Marekani kwa kujitokeza na kujitolea kusaidia katika uchunguzi wa kifo cha mwanaharakati wa LGBTQ Edwin Chiloba.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii, mbunge huyo alisema kuwa jamii imepata hasara kubwa kutokana na kifo cha mwanaharakati wa LGBTQ aliyeuawa.

Passaris aliongeza kwamba tunapaswa kuunda jamii inayojumuisha wote ambapo kila mtu anakubalika na pia kutibiwa kwa usawa.

Pia aliongeza kuwa watu wachache sana katika jamii wanaweza kuweka vichwa vyao juu na kupigania haki za Jumuiya ya LGBT jinsi Edwin Chiloba alivyofanya.

Haya yanajiri baada ya serikali ya Marekani pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kulaani mauaji ya kikatili ya Edwin Chiloba wakiitaka serikali kuharakisha uchunguzi wake.

"Asante @Dept . Kifo cha Chiloba ni hasara kubwa kwa jamii. Ni wachache sana wanaoweza kuweka vichwa vyao nje na kutetea kwa ujasiri haki za LGBTQ kama alivyofanya. Sote tunapaswa kujitahidi kuunda jamii iliyojumuisha zaidi na inayokubalika ambapo kila mtu anatendewa kwa utu na usawa,"Passaris Alisema.

Upasuaji wa maiti ulibaini kwamba Chiloba aliaga dunia kwa kukosa hewa, huku mwanapatholojia akifichua kwamba alikuwa amewekwa soksi mdomoni mwake.