Michelle Ntalami amjibu Sonko baada ya kudai alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Chiloba

Hii ni baada ya kusambaza picha za Edwin Chiloba na anayedaiwa kuwa mpenziwe ambazo zimeibua hisia mtandaoni.

Muhtasari
  • Kwa mujibu wa Sonko, Chiloba inadaiwa alikuwa akitoka kimapenzi na Michelle Ntalami kabla ya kifo chake
Michelle Ntalami amuomboleza Chiloba
Michelle Ntalami amuomboleza Chiloba
Image: Instagram

Aliyekuwa gavana Mike Mbuvi Sonko, amewaacha Wakenya wakizungumza kwenye mitandao tofauti ya kijamii.

Hii ni baada ya kusambaza picha za Edwin Chiloba na anayedaiwa kuwa mpenziwe ambazo zimeibua hisia mtandaoni.

Kwa mujibu wa Sonko, Chiloba inadaiwa alikuwa akitoka kimapenzi na Michelle Ntalami kabla ya kifo chake.

"Kumbe the late Edwin Chiloba had an affair with Michelle Ntalami na walikuwa na mapenzi moto moto hadi jana Michele had to pen down a beautiful tribute to the late Edwin Chiloba recalling the first time they met and the beautiful moments they shared. Rest in Peace Edwin,"Sonko Aliandika.

Sasa, picha hizi za Chiloba na Michael Ntalami wakiwa pamoja, zimesambaa kwenye mitandao tofauti ya kijamii ambapo, zinazua hisia tofauti kwa sasa.

Wengi wanajitokeza kusema kuwa Sonko siku hizi anakuwa mwanablogu makini huku wengine wakiuliza kwa nini Ntalami ikiwa ni kweli alikuwa kwenye uhusiano na Chiloba kama Sonko anavyodai wakati huo huo.

Huku Michelle akijibu madai yake Sonko alisema;

"Eish Michelle hili,MIchelle lile yuko kwenye midomo ya kila tu kwa ajili ya kusihi maisha yake,nini hicho kunihusu ambacho kinawapendeza sana

Inakaa nyinyi nyote mna mengi a kushiriki nami,wacha nifungue sanduku la maoni ndio nyinyi nyoye mfungue roho na mimi

DMs naona zishaanza kujaa wanaorusha mistari kuweni wapole nitaangalia jumbe zenu,Hata wewe MikeSonko najua hilo ndilo lilikuwa haja yako kuu,"Aliandika.