Bingwa wa NBA Shaquille O'Neal alazimika kula chura 'live' kwenye TV kwa kupoteza bet (Video)

O'Neal alisema kuwa timu yake ingepigwa, angeridhia kula chura, ahadi ambayo alitimiza mubashara runingani.

Muhtasari

• O'Neal alikuwa amewekeana miadi na mwenzake Earnie Johnson kwenye runinga wakichambua mchuano wa vikapu.

Shaquille O'Neal, staa mkongwe wa wa mpira wa vikapu America, NBA alilazimika kula chura mubashara runingani baada ya kupoteza ubashiri wake kwa mkeka wa bet ambayo aliweka na mwenzake.

Jarida la CBS linaripoti kuwa Kabla ya mchezo wa Jumatatu wa Mchujo wa Kitaifa wa Soka ya Chuoni, O'Neal alimwekea dau mshiriki wa jopo "Ndani ya NBA" Ernie Johnson kwamba timu ya Georgia Bulldogs, haingewashinda Texas Christian University's Horned Frogs (TCU).

Wawili hao waliafikiana kuwa iwapo timu ya mpira wa vikapu ya Georgia Bulldogs ingeshindwa, basi O’Neal angelazimika kula miguu ya chura moja kwa moja mbele ya kamoera za runinga.

Kwa bahati mbaya kwa bingwa huyo mara nne wa NBA, Horned Frogs walichapwa alama 65-7, Georgia iliposhinda ubingwa wake wa pili mfululizo wa College Football Playoff.

Na kwenye chanjo ya Alhamisi ya TNT ya hatua ya NBA, ulikuwa wakati wa kutimiza ahadi kwa O’Neal.

Earnie Johnson akiwa amevalia kofia ya Bulldogs -- aliingia kwenye seti akiwa ameshikilia sinia ya fedha yenye kifuniko juu yake.

Sinia hiyo ilikuwa na nyama ya miguu ya chura, chakula ambacho alimletea O’Neal ili ale kama kutimiza ahadi yake ya bet waliyowekeana siku chache kabla ya mechi.

Wengi walitarajia kuwa O’Neal angeghairi lakini kwa mshtuko, alionekana akikivamia chakula kile kwa furaha mubashara runingani huku akiramba midomo na kusema kuwa ndicho chakula kizuri zaidi ambacho alikitia kinywani mwake kwa siku nyingi.

"Mimi ni mtu wa neno langu. Nataka tu kukufahamisha, miguu hii ya chura ni nzuri. Hii ndio miguu bora zaidi ya chura ambayo nimewahi kuwa nayo. Hukufikiria ningefanya, sivyo?” O'Neal alisema katikati ya kutafuna.