Gavana Gladys Wanga wa Homabay ampa rais William Ruto zawadi ya ndume

Ruto anaendelea ziara ya kimaendeleo katika mkoa wa Nyanza kwa siku mbili tangu Ijumaa.

Muhtasari

• Homabay ni ngome ya Odinga ya kisiasa kwa muda mrefu.

• Wanga alimkaribisha Ruto kwa mbwembwe na kumuambia kuwa licha ya wao kuwa wa Azimio lakini wanamkubali Ruto kama rais.

Wanga ampa Ruto ndume
Wanga ampa Ruto ndume
Image: Facebook

Ijumaa rais Ruto katika ziara yake ya Nyanza, alitua mwanzo katika kaunti ya Homabay na kulakiwa na gavana wa kaunti hiyo mama Gladys Wanga.

Baadae aliendelea kuzindua mirandi mbalimbali, mingi ikiwa ni ile iliyoanzishwa na serikali iliyopita ya rais Uhuru Kenyatta na mingine ikiwa ni yenye itaanzishwa chini ya uongozi wa serikali yake ya Kenya Kwanza.

Sasa imebainika kuwa gavana Wanga ambaye ni mwandani kabisa wa karibu wa Raila Odinga alimkabidhi rais Ruto zawadi maalum ya ndume.

Rafiki wa Ruto ambaye alikuwa ni kiongozi wa kampeni za mitandaoni za rais, Dennis Itumbi alifichua taarifa hizo kwa kupakia picha ya ndume huyo wa kifahari akiwa ameandikwa kwenye ngozi yake “zawadi ya rais”

Itumbi alisema kuwa ndume huyo ni zawadi iliyotolewa na gavana Wanga kwa rais Ruto kama njia moja ya kumkaribisha katika ngome hiyo ya kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga.

Katika kile ambacho wengi hawakutarajia, rais Ruto alipata mapokezi ya kishujaa wananchi na viongozi wakimkaribisha kwa shangwe na mbwembwe.

Gavana Wanga alimwambia Ruto kuwa hata kama wao ni wanachama damu wa Azimio la Umoja inayoongozwa na Odinga, lakini wanamkubali na kumpenda kama kiongozi wa taifa.

Ziara ya rais katika mkoa wa Nyanza haikuwa ya kisiasa bali safari hii ilikuwa ni ziara ya kimaendeleo na kiongozi wa ODM Raila Odinga aiwarai viongozi na wananchi wote kujitokeza kwa wingi na kuhudhuria ziara hizo kwac siku mbili ambapo Ruto anatarajiwa kuzindua mirando ya kimaendeleo tumbi nzima.