Tanzia: Familia ya waziri Moses Kuria inaomboleza kifo cha dada yake

Rais Ruto alifichua habari hizo kupitia twitter akiiombea familia hiyo neema ya kukubali pigo hilo.

Muhtasari

• "Tunahuzunika pamoja na familia yako na tunakuombea Mola akupe neema ya kuvumilia pigo hili,” rais Ruto aliandika Twitter.

Pauline Nyikabi Kuria, dadake Moses Kuria
Pauline Nyikabi Kuria, dadake Moses Kuria
Image: Twitter

Waziri wa viwanda, uwekezaji na biashara Moses Kuria anaomboleza kifo cha dada yake aliyefariki mapema asubuhi ya Jumamosi Januari 14.

Habari hizo za tanzia zilifichuliwa na rais William Ruto ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter alipakia picha ya mwendazake Pauline Nyokabi Kuria ambaye ni dadake waziri Kuria na kutoa risala zake za rambirambi.

“Rambirambi zetu za dhati ziwafikie mheshimiwa Moses Kuria kwa kumpoteza dada yako mpendwa, Pauline Nyokabi Kuria. Tunahuzunika pamoja na familia yako na tunakuombea Mola akupe neema ya kuvumilia pigo hili,” rais Ruto aliandika Twitter.

Hakuna mengi ambayo yanajulikana kuhusu mwendazake huyo wala kiini cha kifo chake, licha ya nduguye Moses Kuria kuwa na umaarufu mkubwa tangu akiwa mbunge wa Gatundu ya Kusini.

Mwanasiasa huyo ambaye alijaribu kuwania ugavana Kiambu mwaka jana na kubwagwa hajawahi sikika hadharani akizungumzia familia yake na ni wachache sana wanajulikana akiwemo yeye na ndugu yake aliyewania pia ubunge wa Juja ya kuanguka, Aloise Kinyanjui.