Ledama afichua kinachohitajika kufanywa ili Kenya isonge mbele

Kulingana na mbunge huyo mahiri, kuna hitaji la dharura la kuwezesha taasisi huru.

Muhtasari
  • Alisema kuwa ikiwa hili lingeafikiwa basi Kenya itakuwa mahali pazuri bila kesi za miswada inayosubiri kutekelezwa

Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa twitter  Seneta wa Narok Mhe Ledama Ole Kina amezua maoni tofauti mtandaoni baada ya kushauri serikali kuhusu nini cha kufanya ili Kenya isonge mbele.

Kulingana na mbunge huyo mahiri, kuna hitaji la dharura la kuwezesha taasisi huru.

Anashindwa kuelewa kwa nini serikali inazingatia sana mambo mengine badala ya haya.

Alisema kuwa ikiwa hili lingeafikiwa basi Kenya itakuwa mahali pazuri bila kesi za miswada inayosubiri kutekelezwa.

Alimtaka rais ahakikishe kuwa anafadhili mashirika hayo na kuhakikisha kuwa anafuatilia jinsi kaunti zinavyotumia pesa. Alikwenda mbele kumwambia rais kwa uwazi aache ubadhirifu.

"Ili nchi hii isonge mbele lazima tuwezeshe taasisi huru! Miswada hii yote inayosubiri kuwaua Wakenya isingekuwepo kama @CoB_Kenya @PPRA & ya @OAG_Kenya zilifadhiliwa kikamilifu na kuruhusiwa kufuatilia kila matumizi ya kaunti. @WilliamsRuto lazima tuache ubadhirifu!