Wacheni kumwelekeza Rais Ruto la kufanya-DP Gachagua kwa Azimio

DP Gachagua aliongeza kuwa ajenda ya Rais ilikuwa wazi katika mpango wa Kenya Kwanza,

Muhtasari
  • Akizungumza Mombasa mnamo Januari 8, Raila alisema viongozi wanapaswa kukoma kutumia makanisa kama majukwaa ya kisiasa
Naibu Rais William Ruto
Image: TWITTER// RIGATHI GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua ameupinga upinzani akisema wanapaswa kukoma kumwelekeza Rais William Ruto la kufanya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za Ruiru Alhamisi, Naibu Rais alisema muungano wa Azimio umekuwa ukifanya kazi kwa bidii kuamuru ajenda ya Ruto.

"Tunawaambia hawa wahusika wa Azimio. Tafadhali, msijaribu kuweka ajenda ya Rais William Ruto," akasema.

DP Gachagua aliongeza kuwa ajenda ya Rais ilikuwa wazi katika mpango wa Kenya Kwanza, na iliangaziwa kwenye kandarasi ya kijamii na Wakenya.

Huku akionekana kumsuta kinara mkuu wa upinzani Raila Odinga kuhusu matamshi yake kuhusu makanisa kutumika kama majukwaa ya kisiasa, Gachagua alisema Ruto hahitaji ushauri wa mahali pa kuhudhuria ibada au pa kwenda kwa programu za maendeleo.

Akizungumza Mombasa mnamo Januari 8, Raila alisema viongozi wanapaswa kukoma kutumia makanisa kama majukwaa ya kisiasa.

"Tunakuja kanisani kusali na kushirikiana na Wakristo wenzetu," alisema.

“Kama tunataka kuongea siasa tufanye huko nje ya uwanja, wenzetu wamegeuza kanisa kuwa uwanja wa siasa, baada ya ushirika wanatufundisha nini tumefanya na tunachotaka jambo ambalo halikubaliki.