Kisumu: Polisi waokoa watu waliofungwa minyororo kwenye 'seli' kanisani

'Wafungwa' hao walisema huwa wanaruhusiwa kuona jua mara moja kwa wiki na kukaa siku kadhaa bila kuoga.

Muhtasari

• Mchungaji wa kanisa hilo alisema huwa anawafunga kwa kile aliwataja kama wenye matatizo ya akili ili wasishambulie wengine.

Wafungwa kwa minyinyoro
Wafungwa kwa minyinyoro
Image: CBC,

Jumapili runinga ya NTV ilipeperusha Makala yaliyoelezea jinsi baadhi ya waumini katika kanisa moja jijini Kisumu walifungwa wanafungwa katika moja ya chumba cha kanisa hilo kama wafungwa.

Kulingana na ripoti hiyo, wafungwa hao walikuwa ni watu wenye matatizo ya akili ambao walikuwa wamefungiwa kwa lengo ambalo lilikisiwa ni kuitishiwa maombi kutoka kwa Mungu wakiwa kifungoni.

Baadhi ya waathiriwa hao waliogeuzwa wafungwa walisimulia jinsi walikuwa wanapitia magumu mikononi mwa watumishi wa Mungu.

Kando na kugawana seli, hutumia ndoo kujisaidia. 'Wafungwa' wanaruhusiwa tu kuona jua mara moja kwa wiki. Mtu mwingine ambaye alizuiliwa kanisani alisimulia jinsi alivyonusurika bila kuoga kwa majuma kadhaa.

"Tangu nitoke chumba kingine sijawahi kuoga, hadi jana nilikuwa naomba maji lakini hakuna aliyekuwa akinisikiliza," mmoja wa wagonjwa waliowekwa kizuizini alisema kama ilivyoripotiwa na NTV.

Ripoti hiyo haikukamilika pasi na kupata tamko la mchungaji wa kanisa hilo ambaye alitambulika kama John Pesa.

Kulingana naye, watu hao waliokuwa wamezuiliwa walikuwa na matatizo ya akili huku akitetea kuzuiliwa kwao ndani ya ‘seli’ kwa kusema kuwa hatua hiyo huwa inalenga kuwazuia dhidi ya kuwashambulia waumini wengine wanaoenda kanisani hapo kwa ibada.

"Hutarajii tuwaache watu hawa wazururaji kwa uhuru lakini wengine wana matatizo ya afya ya akili. Wanapaswa kufungwa minyororo ili wasiwashambulie watu wengine walio karibu nao, Hata hivyo, wanapotulia kidogo, tunaondoa minyororo,” Pesa alisema.