Gavana Sakaja: Nitafanikisha Handshake ya Ruto na Odinga, Sijuti kufanya kazi na wote

Sakaja alikuwa katika kambi ya Odinga miaka ya nyuma kabla ya kumtoroka na kujiunga TNA cha Uhuru Kenyatta.

Muhtasari

• Haya yanajiri wakati ambapo viongozi hao wawili kila mmoja amefutilia mbali uwezekano wa kufanya handshake.

Sakaja aapa kuleta handshake baina ya Odinga na Ruto
Sakaja aapa kuleta handshake baina ya Odinga na Ruto
Image: Twitter

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameampa kufanikisha maridhiano baina ya rais William Ruto na mpinzani wake wa kisiasa Raila Odinga.

Katika video ambayo sasa imeenea pakubwa kwenye mitandao ya kijamii, Sakaja anasikika akisema kuwa hawezi kujuta kufanya kazi na Raila Odinga wala kufanya kazi na William Ruto kwa sasa.

Sakaja alianza siasa zake katika kambi ya kinara wa ODM Raila Odinga kabla ya kumtoroka mwaka 2013 na kujiunga na TNA chake Uhuru Kenyatta ambaye baadae walishikana na Ruto kuunda Jubilee.

Sakaja anasikika akitetea hatua yake kuwa Nairobi ni kaunti ya kila mtu na kwa sababu hiyo, yeye hawezi kuwa na chuki na kufanya na mtu yeyote baina ya viongozi hao wawili ambao tangu uchaguzi wa mwaka jana wamekuwa watu wa kutoonana jicho kwa jicho.

“Sina msamaha wowote kwa kufanya kazi na Raila Odinga, na pia sina msamaha kwa mtu yeyote kwa kufanya kazi na William Ruto. Na kusema kweli ilec siku William Ruto na Raila Odinga wataketi, mimi ndio nitawaleta pamoja wakae kwa meza. Kwa sababu Nairobi si ya mtu yeyote, si ya kabila lolote, si ya chama chochote, ni ya watu wote wa Nairobi. Rais wetu apewe heshima yake, lakini pia Raila Amollo Odinga, mhandisi,” Sakaja alisikika akisema.

Maneno ya Sakaja kufanikisha Handshake baina ya Odinga na Ruto yanakuja siku moja tu baada ya rais Ruto kusema hawezi kubali kufanya handshake na kinara huyo wa upinzani katika kile alisema kuwa anataka kuwe na upinzani mkali kwa serikali yake.

Odinga pia alikanusha jana kuwa hataki Handshake na rais Ruto, huku akisema hawezi kutambua uongozi wake katika kile alisema aliibiwa kura katika uchaguzi wa mwaka jana.