Bungoma: Mzee wa miaka 78 asimulia kung'atwa nyeti zake na mke wa kijana wake

"Nilienda kusuluhisha ugomvi, binti mkwe akanipiga jiwe mgongoni nikaanguka, akakimbia na kuniangukia kabla ya kuniuma nyeti."

Muhtasari

• Mwanamke huyo alimpiga jiwe la mgongoni baba mkwe kabla ya kumuangukia na kuanza kumuuma sehemu zake za siri.

• Baadae alielekea kwa nyumba akitaka kuchoma vitu lakini polisi wakamdhibiti.

Mzee wa miaka 78 aliyeshambuliwa na binti mkwe
Mzee wa miaka 78 aliyeshambuliwa na binti mkwe
Image: Screengrab//Citizen

Mzee mmoja kutoka kaunti ya Bungoma ameelezea kisa cha ajabu jinsi mke wa kijana yake alimshambulia kwa kumuuma sehemu zake za siri alipojaribu kutatua mgogoro wa ndoa ya mtoto huyo wake.

Mzee huyo alisimulia kwamba ilikuwa ni tarehe 28 mwendo was aa kumi ambapo alikuwa anakula chakula chake cha jioni.

Mzee huyo wa miaka 78 ambaye mke wake alifariki miaka kadhaa nyuma alisema kuwa alipokuwa akila chakula, alisikia kelele kutoka kwa jirani ambapo aliitwa akafahamishwa kwamba mke wa kijana yake ndiye alikuwa anavurugana na mwanamke mwingine kwa tuhuma za kuchukua mume wake – kijana wa huyo mzee.

Mzee huyo alichukua fimbo yake akajikokota na kusikiliza mgogoro huo ambapo alijaribu kuzungumza na mke wa mtoto wake lakini ikashindikana kwa vile mwanamke huyo alikuwa amepandwa hasira kuliko za mkizi.

Alipoona juhudi zake za kuleta utulivu zimegonga mwamba, aliamua kurudi kwa nyumba yake lakini yule mwanamke akachukua jiwe na kumgonga kwa mgongo hadi kumuangusha chini.

Baada ya kuanguka chini, mzee alisema kuwa mwanadada huyo alikimbia na kumuangukia kifuani na baadae kuanza kumvua suruali huku akitia meno yake kwenye uume wake.

“Nilipoona hataki kupoa nikasema acha mimi nirudi, kumbe alikuwa na hasira, akachukua mawe na kunipiga kwa mgongo. Nikaanguka chini nikakosa fahamu, mke wa mtoto wangu akaniangukia, ni mkwe wangu, akaniuma nikajaribu kumsukuma hapo ndio alinishika suruali, hakunitoa. Alikunja suruali hapa mbele kwa zipu na kuweka kwa mdomo wake na akaniuma ukweli. Nikalia. Mtoto wangu ndiye alikuja akanisaidia,” mzee huyo alielezea.

Baadae mkwe huyo wake alielekea kwa nyumba yake akisema kuwa anataka kuua mtoto baada ya kuchoma vitu vyote kwa nyumba.

Polisi waliitwa wakafika haraka ambapo walimweka chini ya ulinzi na mzee akatafutiwa usafiri wa pikipiki kuelekea kituo cha polisi kuandikisha ripoti ya kuvamiwa na mkwe wake.