Mwendawazimu amvamia mwanamke kanisani akifanya maombi, ampiga mawe hadi kufa

Mwendawazimu huyo alikuwa ameletwa kanisani kwa ajili ya maombi, ghafla alitoka nje na kurudi na matofali mikononi.

Muhtasari

• Polisi walifika katika eneo hio la kuabudu na kumtia nguvuni kichaa huyo huku mwili wa mwanamke ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

crime scene
crime scene

Polisi katika kaunti ya Migori, Kuria Magharibi wanachunguza kisa cha kushangaza ambapo mwanamume analiyetajwa kuwa mwenye akili punguani kumshambulia kwa mawe mwanamke mmoja kanisani.

Inadaiwa kwamba mwanamke huyo kwa jina Pamela Akumu alienda kanisani kwa ajili ya ibada ya maombi ambapo mwendawazimu huyo ambaye alifika kanisani baadae na kumshambulia kwa mawe hadi kumuua.

Kulingana na taarifa za polisi huko Isebania, mama huyo alikuwa ameenda kushiriki ibada ya maombi ya jioni, na mule kanisani mwendawazi aliletwa na mamake pia kwa ajili ya maombi. Kichaa huyo alitoka nje na kurudi akiwa na matofali ambayo alitumia kumshambulia Akumu na kumuua papo hapo.

Baadhi ya waumini walifanikiwa kutoroka huku Akumu ambaye alikuwa ajuza wa miaka 66 akizidiwa na mashambulio ya mawe kichwani hadi kufa.

Maafisa na wapelelezi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) walifika eneo la tukio na kukuta mwili huo ukiwa nje ya kanisa ukiwa na majeraha mabaya kichwani.

Matofali mawili yalitolewa kwenye eneo la tukio na kuwekwa kama ushahidi.

“Mshukiwa alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi. Hatua za lazima zilichukuliwa na mwili huo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mtakatifu Akidiva Mindira Mabera ukisubiri uchunguzi wa upasuaji wa maiti,” ilinukuliwa sehemu ya ripoti hiyo na kuongeza kuwa kwa sasa kesi hiyo iko mahakamani.

Haya yanajiri wakati kule Nairobi kisa sawia na hicho kiliripotiwa katika eneo la Dagoretti ambapo majirani walimshambulia kwa mawe mlevi mmoja aliyeingia nyumba ya jirani akidhani ni kwake.

Jirani yake ambaye ni mwanamke alipiga kelele kuita usaidizi ambapo majirani waliwahi kwa haraka na kumshambulia mlevi huyo wakidhani ni mhalifu na mbakaji.

Polisi walifika na kumuokoa lakini alifariki hospitalini akipokea matibabu.