Wacha wapige mdomo-Uhuru amjibu Ruto kuhusu kutuhuma za ufadhili wa Raila

Alizungumza alipoandamana na Uhuru hadi nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Elimu George Magoha

Muhtasari
  • Mnamo Jumanne, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alielezea wasiwasi wake kwamba mtu yeyote angetaka kumdhulumu Uhuru
Image: WILFRED NYANGARESI

Rais wa zamani Uhuru Kenyatta amepuuza wasiwasi kwamba serikali ya Kenya Kwanza inalenga kumdhulumu.

Mnamo Jumanne, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alielezea wasiwasi wake kwamba mtu yeyote angetaka kumdhulumu Uhuru.

Huku akiiifariji familia ya marehemu Magoha, aliotumia fursa hiyo na kumjibu Rais Ruto.

"Na wewe Steve usijali hii watu wanapiga mdomo, wacha wapige bwana. Unajua mtu ambaye hana kitu ingine ya kufanya lazima apige mdogo, wacha wapige bwana, hiyo ni ya dunia, sisi tunaendelea na yetu," Uhuru alisema.

Kalonzo alisema amekuwa katika siasa kwa muda mrefu na ameshuhudia mabadiliko ya mamlaka kutoka kwa mwanzilishi Jomo Kenyatta hadi Uhuru Kenyatta na hakukuwepo tatizo au kulipiza kisasi.

"Nilimwona Mzee Moi akichukua hatamu kutoka kwa Mzee Kenyatta na hatimaye Mzee Kibaki akachukua hatamu kutoka kwa Mzee Moi, unajua, mabadiliko ya bila mpangilio na bila kutaja majina," Kalonzo alisema.

Alizungumza alipoandamana na Uhuru hadi nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Elimu George Magoha mtaani Lavington Nairobi ili kuwapa pole familia hiyo.

Kalonzo alisema baada ya Moi kustaafu, baadhi ya watu katika Baraza la Mawaziri walitaka anyang'anywe nyumba yake ya Kabarnet Gardens jijini Nairobi, lakini wazo hilo lilifutiliwa mbali na aliyekuwa rais Mwai Kibaki.