'Kila mtu ananialika harambee,'DP Gachagua asema baada ya kurudishiwa pesa zake

Akizungumza siku ya Alhamisi Gachagua aliyeonekana mwenye furaha alichukua muda wa kuichunguza serikali iliyopita

Muhtasari
  • DP alisema kwamba yuko tayari kufanya kazi na wansiasa wa mirengo yote, ili kutimiza matakwa ya Wananchi
Naibu Rais William Ruto
Image: TWITTER// RIGATHI GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua anasema kwa muda wa saa 24 zilizopita amepokea zaidi ya mialiko 200 ya kuhudhuria hafla ya kuchangisha pesa baada ya pesa taslimu yake ya Ksh.200 milioni ambayo serikali ilikuwa imepokonywa na serikali kurejeshwa kwake.

Akizungumza siku ya Alhamisi Gachagua aliyeonekana mwenye furaha alichukua muda wa kuichunguza serikali iliyopita, akisema kuwa pesa zake "zilizochukuliwa na serikali ya Uhuru" zimerudishwa kwake na kwamba kila mtu sasa kupigania sehemu ya mkate.

"Leo asubuhi nimepokea mialiko zaidi ya 200 ya kuhudhuria harambee. Serikali ya Uhuru ilikuwa imechukua pesa zangu na zilitolewa jana. Sasa kila mtu anapangia pesa hizo. Hiyo ndiyo dunia tunayoishi...," alisema Gachagua.

Aliongeza: "Kila mtu ananialika harambee kwa sababu inaonekana kama pesa nyingi."

Gachagua alikuwa amepoteza Ksh.200 milioni za fedha zilizozuiliwa na mahakama kwa Serikali mwishoni mwa Julai mwaka jana baada ya Mahakama Kuu kuamua kuwa hangeweza kuthibitisha jinsi alivyopata pesa hizo.

DP alisema kwamba yuko tayari kufanya kazi na wansiasa wa mirengo yote, ili kutimiza matakwa ya Wananchi.

“Mimi ni mtu rahisi sana wale ambao hawapo pamoja nasi msiamini mnachosoma kwenye mitandao ya kijamii kunihusu, nimetoka mbali hadi sasa ambapo Mungu ameniweka, mimi ni mtu mnyenyekevu sana unaweza njoo ofisini kwangu wakati wowote tunapozungumza. Ninasikiliza kwa makini na kuheshimu maoni ya kila mtu," DP Gachagua alisema.

Gachagua alionekana kumrushia rais mstaafu vijembe huu akimwambia kwamba lazima alipe ushuru.