Nairobi watu 2 tu wataenda mbinguni!: Seneta Sifuna ataka kukutana na Yesu wa Tongaren

Seneta Sifuna alionesha haja yake ya kutaka kukutana na jamaa huyo kujua ni akina nani hao wawili.

Muhtasari

• Yesu wa Tongaren alisema duniani kote idadi ya waqtu 168K pekee ndio wataenda mbinguni, idadi hiyo ikijumuisha wawili tu kutoka Nairobi.

Yesu wa Tongarn asema watu 2 pekee kutoka Nairobi wataenda mbinguni, Sifuna ataka kukuana naye
Yesu wa Tongarn asema watu 2 pekee kutoka Nairobi wataenda mbinguni, Sifuna ataka kukuana naye
Image: Facebook

Seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna ametangaza azma yake ya kutaka kukutana na mhubiri kutoka kaunti ya Bungoma kwa jina Yesu wa Tongaren, baada ya jarida la Taifa Leo kuripoti kuwa alitoa ufunuo kuhusu kaunti ya Nairobi.

Kulingana na mchungaji huyo, watu wawili pekee kutoka kaunti ya Nairobi ndio wataenda mbinguni, huku watu wapatao elfu 168 kote duniani wakiwa ndio wateule pekee wa kwenda mbinguni.

Tamko lake kuwa watu wawili tu kutoka kaunti ya Nairobi ndio watakuwa miongoni mwa laki moja elfu sitini na ushee kote duniani, lilimchochea seneta wa kaunti hiyo yenye zaidi ya wakaazi milioni 4 akisema ana uchu wa kukutana naye moja kwa moja ili kubaini ni akina nani hao wawili ambao wamepata upako wa kuteuliwa kwa msafara wa halaiki ya watakaoelekea kweney malango ya peponi.

“Ati watu wawili pekee, nahitaji kuzungumza na huyu jamaa,” seneta Sifuna alisema huku akiweka emoji ya kucheka.

Yesu wa Tongaren, kama anavyojiita mchungaji huyo aliyedai kutojua jina lake halisi zaidi ya hilo, aligonga vichwa vya habari mwezi jana aliponukuliwa akidai kuwa yeye ndiye Yesu ambaye watu wamekuwa wakisoma kweney vitabu vitakatifu kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Mchungaji huyo ana wanafunzi zaidi ya 12 ambao ni kama wale aliokuwa nao Yesu Mnazareti, huku pia mke wake kwa jina Nabii Benjamini akijiita mtakatifu aliyebarikiwa zaidi kuliko wanawake wote duniani – kama tu mama wa yesu – Bikira Maria.