Mwambie Uhuru azungumze na wanachama wa Jubilee-Ledama kwa Kioni

Katika mkutano wa Jumatano, wabunge wa Jubilee waliahidi kufanya kazi na kuunga mkono serikali.

Muhtasari
  • "Tunataka kuwa sehemu ya serikali hii tukiwa pamoja kabla ya uchaguzi uliopita," Mbunge wa Eldas Adan Keynan alisema
LEDAMA 2
LEDAMA 2

Seneta wa Narok Ledama Olekina amewataka viongozi wa chama cha Jubilee kuzungumza na wanachama wake.

Akizungumza Jumatano, Olekina alisema kuwa katibu mkuu Jeremiah Kioni anafaa kuwasiliana na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, ambaye ni kiongozi wa chama cha Jubilee.

"Jeremiah Kioni. Tafadhali mwombe Uhuru aje kuzungumza na wanachama wako," alisema.

Kauli yake inajiri wakati Rais William Ruto alifanya mkutano na wabunge 32 kutoka chama cha Jubilee.

Hii ni mara ya pili kwa wajumbe hao kukutana naye Ikulu mwaka huu.

Katika mkutano wa Jumatano, wabunge wa Jubilee waliahidi kufanya kazi na kuunga mkono serikali.

"Tunataka kuwa sehemu ya serikali hii tukiwa pamoja kabla ya uchaguzi uliopita," Mbunge wa Eldas Adan Keynan alisema.

"Kwa kiwango hiki, tutafunga jumba letu la Jubilee na kuungana nanyi kwa sababu sisi ni wamoja," Mbunge wa Laikipia Kaskazini Sarah Korere alisema.