Silas Jakakimba, msaidizi wa Raila Odinga amtuhumu Winnie Odinga kwa kumtukana

"Winnie alinitumia ujumbe wa matusi yanayoanza na herufi F kwa sababu tu nimetumia picha ya Ruto kwenye jalada langu," - Jakakimba.

Muhtasari

• Alimtaka Winnie kuwaheshimu watu ambao wako karibu na baba yake kwani wamepitia mambo magumu sana mpaka kupata uaminifu wake.

Silas Jakakimba amtuhumu Winnie Odinga kwa kumtukana.
Silas Jakakimba amtuhumu Winnie Odinga kwa kumtukana.
Image: Facebook

Silas Jakakimba, msaidizi wa muda mrefu katika ofisi ya Kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga ametoa tamko la kutupa lawama kwa binti wa kinara huyo Winnie Odinga kwa kile alisema kwamba ni kumkosea heshima.

Jakakimba kupitia ukurasa wake wa Twitter, ametumia picha ya rais William Ruto akisalimiana kwa tabasamu na viongozi wengine wa Nyanza, picha ambayo alisema ilimfanya Winnie kumtupia matusi ya nguoni yanayoanza na herifu f**** katika lugha ya kimombo.

Jakakimba ambaye alionekana kughadhabishwa na tamko hilo la mbunge wa EALA Winnie alimtaka binti huyo wa Odinga kutambua kwamba wao wanamheshimu sana baba yake na yeye anafaa kuwaheshimu pia wanaofanya kazi kwa ukaribu na yeye.

“WINNIE ODINGA alinitumia tusi la F jana usiku kwa kile anachosema usaliti badala ya Picha yangu ya Jalada. Anachoshindwa kuthamini: Tunaheshimu JAKOM nimeyofanywa NUSU ya Miaka ya Maisha yangu karibu na yeye na ikiwa anaJALI kujua, tumekuwa tukipitia tanuru ngumu ya mtoto kujitolea kwa ajili ya uaminifu huo,” Jakakimba alisema.

“Ni muhimu kusonga mbele kwamba Winnie ajifunze kuheshimu watu jinsi walivyo - ikiwa sivyo, kwa yale ambayo wamekuwa katika safari ndefu ya hali ya chini na ya juu sana, kwa upendo wa Nchi,” aliongeza.

Kuelekea uchaguzi wa mwaka jana, Jakakimba alisemekana kuwa alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wanawania tikiti ya ODM kuwania ubunge wa Lang’ata lakini baadae alijiondoa katika kinyang’anyiro cha mchujo.