Ruto hana heshima kwa katiba - Boniface Mwangi adai

Hata hivyo, Rais William Ruto mara kadhaa amewahakikishia Wakenya kwamba utawala wake utaongozwa na sheria.

Muhtasari
  • Akizungumza siku ya Alhamisi, Mwangi alidai kuwa Ruto anataka kutawala kwa mabavu na kwamba anaogopa siku zijazo.
RAIS WILLIAM RUTO
Image: KWA HISANI

Mwanaharakati Boniface Mwangi amemshutumu Rais William Ruto kwa kutoheshimu Katiba ya Kenya.

Akizungumza siku ya Alhamisi, Mwangi alidai kuwa Ruto anataka kutawala kwa mabavu na kwamba anaogopa siku zijazo.

Aliendelea kumfananisha Ruto na hasimu wake Raila Odinga, ambapo alisema kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani ana dosari zake lakini angalau anaheshimu Katiba.

"Licha ya udhaifu mwingi wa Raila Odinga, anaheshimu katiba yetu. Familia ya Odinga imelipa gharama kubwa ya kibinafsi kwa Kenya kuwa na utawala wa sheria. Ruto hana heshima kwa katiba, anataka kutawala kwa amri na sifa. . Ninaogopa siku zijazo," Mwangi alisema.

Matamshi yake yalifuatia ghasia za baadhi ya Wakenya kuhusu uteuzi wa Makatibu Wakuu watawala.

Hata hivyo, Rais William Ruto mara kadhaa amewahakikishia Wakenya kwamba utawala wake utaongozwa na sheria.

Pia matamshi yake yanajiri huku kukiwa na shinikizo kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini, Rais Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wafanye mazungumzo kwa manufaa ya Wananchi.

Wito wa viongozi hao ulijiri baada ya kinara huyo wa ODM kutangaza kuwepo kwa maandamano JUmatatu na Alhamisi kila wiki.