Mike Sonko awashauri 'side chicks' kuwa na subira na waume wao

Aliwahimiza kushikamana na wanaume wao na sio kuwaacha.

Muhtasari
  • Mamilioni ya watu walifuatilia tukio hilo kote ulimwenguni. Tukio hili limepangwa kwa zaidi ya miezi minane.
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amewashauri mipango wa kando kuwa na subira na wanaume wao.

Aliwahimiza kushikamana na wanaume wao na sio kuwaacha.

Mike Sonko alikuwa akimrejelea Camila ambaye ni mke wa Mfalme Charles.

Mfalme mpya wa Uingereza alitawazwa leo(Jumamosi) katika hafla ya kimataifa iliyohudhuriwa na viongozi wa ulimwengu.

Camila alikuwa mpenzi wa Mfalme Charles kwa miaka mingi. Walianza kuchumbiana hata wakati Charles alikuwa bado amemuoa na Princess Diana. Baadaye walifunga ndoa mnamo 2005.

Mfalme Charles alitawazwa katika sherehe ya kupendeza huko London.

Mfalme anachukua nafasi ya mamake Malkia Elizabeth aliyefariki mwaka jana. Alikuwa mfalme aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.

Viongozi kadhaa wa dunia akiwemo rais wa Kenya William Ruto walihudhuria hafla hiyo.

Mamilioni ya watu walifuatilia tukio hilo kote ulimwenguni. Tukio hili limepangwa kwa zaidi ya miezi minane.

Sonko alisema;

"KWA WOTE SIDE CHICS. Ninataka tu kukuhimiza popote ulipo, amini tu na kuwa mwaminifu kwa wanaume wako. Leo, mwenzako/aliyekuwa chic, Camila ni Malkia Consort wa Uingereza. She was Prince Charles' side chic ambaye baadae alifunga ndoa rasmi na Prince mwaka wa 2005 baada ya marehemu Princess Diana kuanza kuhangaika na kupigwa mangwa na kupigwa ma quickie mpaka kwa magari."