Kwa nini rekodi ya kupika kwa saa 100 ya mpishi wa Nigeria haijatambuliwa na Guinness?

Mrembo huyo alipika mapishi zaidi ya 250 kwa saa 100 mfululizo bila kupumzika na kuvunja rekodi ya awali ya saa 87 iliyowekwa mwaka 2019 na raia wa India.

Muhtasari

• Rekodi ya "marathon ndefu zaidi ya kupikia na mtu binafsi" ilivunjwa na Baci, ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii.

• Mpishi alishinda alama ya awali ya Lata Tondon ya saa 87 na dakika 45 Jumatatu asubuhi; Tondon si tena mmiliki wa Rekodi ya Dunia ya Guinness.

Hilda Baci, mpishi wa Nigeria aliyepika kwa saa 100 mfululizo.
Hilda Baci, mpishi wa Nigeria aliyepika kwa saa 100 mfululizo.
Image: Instagram

Guinness World Record wametoa sababu zao za kutoidhinisha rekodi mpya ya mpishi wa Nigeria Hilda Baci (Hilda Effiong Bassey) ya saa nyingi zaidi alizotumia kupika Jumatatu.

Rekodi ya "marathon ndefu zaidi ya kupikia na mtu binafsi" ilivunjwa na Baci, ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii.

Mpishi alishinda alama ya awali ya Lata Tondon ya saa 87 na dakika 45 Jumatatu asubuhi; Tondon si tena mmiliki wa Rekodi ya Dunia ya Guinness.

Hilda alianza changamoto siku ya Alhamisi alasiri kwa kuwasha jiko lake. Hilda ndiye mtu wa kwanza kuwahi kutumia muda mwingi kupika na anapika kwa saa nyingine 96 baada ya kuvunja rekodi ya awali.

Hata hivyo, Guinness World Records ilitangaza kwamba itachambua kwanza uthibitisho wote kabla ya kuthibitisha rasmi rekodi hiyo.

Mtumizi mmoja kwa jina AlexanderDGreat kwenye Twitter alihoji kwa nini rekodi mpya ya Hilda haikutajwa na Guinness World Records.

"Kwa nini Rekodi ya Dunia ya Guinness haionyeshi au kuzungumza juu ya mpishi Hilda? Sijawezi kuona chochote kwenye kurasa zao (Twitter, Facebook, YouTube),” alitweet.

Kwa kujibu, GWR ilisema; "Tunafahamu kuhusu jaribio hili la ajabu la rekodi, tunahitaji kupitia ushahidi wote kwanza kabla ya kuthibitisha rasmi rekodi".

Mpikaji huyo alianza Mei 11 na kumalizika Mei 14. Ilikuwa na kipindi kilichotiririshwa moja kwa moja kwenye chaneli nyingi za mitandao ya kijamii ambapo Hilda alitengeneza mapishi zaidi ya 250 na hatimaye kumpa sifa ya kujivunia kuhusu rekodi ya dunia.

Hilda hapo awali alipita rekodi ya hapo awali iliyowekwa na Lata Tondon, mpishi wa India, mnamo 2019.

Lata Tondon alipika kwa saa 87, dakika 45 na sekunde 00 ili kuvunja rekodi ya awali.

Hata hivyo, Hilda aliweka rekodi mpya saa nane mchana. Jumatatu, Mei 15, 2023.

Alipika kwa saa 100 ili kuweka Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa saa ndefu zaidi za kupikia na mtu binafsi.

Baci alianza mashindano yake ya mbio za marathon siku ya Ijumaa katika bustani ya Amore, Lekki, Jimbo la Lagos.