Hakuna kitu tamu kama kukula fee-MCA Wambui akiri kula karo akiwa chuo kikuu

Wambui amesema kwamba alifurahia sana kula karo, ambayo alikuwa ametumiwa na baba yake.

Muhtasari
  • Aliendelea na kusema kuwa kwa sasa ni mzazi na anamatumaini kwamba mwanawe hatafanya kitendo kama hicho alichokifanya.
MWAKILISHI WADI SHARLEEN WAMBUI
Image: FACEBOOK

Mwakilishi wadi wa kaunti ya Murang'a Sharleen Wmbui amezuo gumzo mitandaoni baada ya kukiri kula karo ya shule alipokuwa katika chuo kikuu.

Wambui amesema kwamba alifurahia sana kula karo, ambayo alikuwa ametumiwa na baba yake.

"Kuna siku dad sent me school fees nikalipe nikiwa campus like twice nikakula. Let me tell you, hakuna kitu tamu kama kukula fee wueh! Very sweet!! ushawahi kula fee?"MCA huyon aliwauliza wafuasi wake.

Aliendelea na kusema kuwa kwa sasa ni mzazi na anamatumaini kwamba mwanawe hatafanya kitendo kama hicho alichokifanya.

"Sahii mimi ndiyo mzazi am just hoping My Amira will not do the same 🥲🥲 you know atleast my dad has shock absorbers na mimi sina!! Na msiniambie ya dunia inalipwa hapa hapa because some comments will disappear mysteriously..🤫."

Ujumbe wake ulileta hisia tofauti kwenye ukurasa wake wa facebook huku baadhi yao wakitoa na kufichua jinsi waliwahi kula karo ya shule na hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao;

Philip Kiptoo: Nliwahi bet nayo na hivo nliscam pesa ya nyumba miezi mbili na kuhama ndio nilipie fee 😂😂

Laban Njeri Thuo: 🤣🤣🤣🤣🤣 she might not maliza yoote but am sure atakula na akucon by that time utakuwa governor nîkîî weeee

Lilian W Ngenia: Aki mboba sikuwai kula fees? Seems wale wote walikula wazazi wao walikua na madooooow ju singeimagine vile mum anahustle alafu nikule fees that would have been the end of me and graduation.Ata highschool nilijilipia yote nilikua natumwa nazo equity ka nimewekewa katikati ya text book ndio mtu adhanie naenda tuition.I was so focused with life ata ka kiliniramba🤣🤣🤣🤣

Carol Benz: Nilikula remedial money alafu nikagonjeka shule dad akaitwa before niandikiwe leave out sheet akasema aonane na classteacher.......niliskia class teacher akisema baba Caroline I was to call you sijaona remedial ya 2 terms na umekua ukisema utaleta in two weeks let me tell you Maina ata mzae hakungoja mwalimu amalize nilionwa war nkapona🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Monica Johnson: Hata mi nimekula once high school na twice campus. Lol feels bad now. I hope my son doesnt.

Denice Babake: Ata kama sio school fees itakuliwa bora tuh utapatikana....