MIGUNA MIGUNA AREJEA

Miguna Miguna amkosoa Ruto kuhusu kutoza ushuru

Kupitia kutozwa ushuru demokrasia huibua mhemko kwa mazingira duni ya watu

Muhtasari

•Wakili katika mahakama ya juu Dkt. Miguna Miguna amejitokeza na kumkosoa rais Ruto kutokana na jinsi ananvyopigia debe kutozwa ushuru kwa Wakeya

Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Image: Andrew Kasuku

Wakili katika mahakama ya juu Dkt. Miguna Miguna amejitokeza na kumkosoa rais Ruto kutokana na jinsi ananvyopigia debe kutozwa ushuru kwa Wakeya.

Katika mtandao wake wa Tweeter,Miguna alisema  ni vyema kuuchunguza mswada kiukweli na wala si kwa kuzingatia hekaya.“La. Nasema chunguza mswada kiukweli,si kwa hekaya.Pili, nadakia kwamba ni kupitia ushuru ambapo demokrasia kuchangia mhemko wa ubepari kutoka kwa viumbe wanaoishi katika mazingira duni.”

Miguna Miguna amekuwa mshauri mkuu wa kiongozi wa upinzani muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga tangu mwaka wa 2017.Itabakia kama kumbu kumbu za historia katika uchaguzi mkuu wa 2017 alivyoendeleza maandamano ya kupinga matokeo ya wakati huo Uhuru Kenyatta.

Pia,Miguna Miguna amekuwa kiongozi wa chama ya National Resistance Movement, chama cha upinzani kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga ijapokuwa kuwa chama hicho kiliharamishwa na serikali 2018. Wakili Miguna pia anakumbukwa kwa kumlisha kiapo cha ofisi Raila Odinga Januari 30, 2018 wakati ambapo juhudi za kuchukua uongozi ziligonga mwamba licha ya uchaguzi mkuu kurudiwa.

Haya yalichangia kulazimishwa kuondoka nchini,alipopeleka mafichoni kwa kukinzana na kipengele ya katiba na sheria za nchi.