Polisi apewa kichapo cha mbwa koko msikitini kwa kupatikana na ng'ombe aliyeibwa

Polisi huyo aliviziwa akimshusha ng'ombe huyo kwa gari la polisi akimpeleka mtoni.

Muhtasari

• Inaarifiwa kwamba afisa huyo aliviziwa na kuonekana akimshusha ng’ombe huyo wa wizi kutoka katika gari la polisi huku akimpeleka mtoni kunywa maji.

• Aliyemuona aliwaita wanakijiji ambao bila kusita walifika kwa makumi chini ya dakika chache kabla ya kuanza kumpakulia polisi huyo adhabu.

Crime Scene
Image: HISANI

Polisi mmoja katika kaunti ya Kakamega alijipata pabaya kwenye mikono ya wananchi wenye ghadhabu baada ya wananchi hao kumfumania akiwa na ng’ombe aliyedhaniwa kuwa wa wizi.

Kulingana na Citizen, wananchi walijawa na ghadhabu baada ya kugundua kwamba ng’ombe ambaye alikuwa ametoweka kwa njia za utata kutoka  boma moja kijijini humo alikuwa mikononi mwa afisa wa polisi.

Baada ya kumkuta na ng’ombe huyo, wananchi walimuangushia kichapo cha mbwamwitu msikitini katika kile kiliripotiwa kuwa ni kumtuhumu afisa huyo wa polisi kutekeleza wizi kwa kutumia dola.

Inaarifiwa kwamba afisa huyo aliviziwa na kuonekana akimshusha ng’ombe huyo wa wizi kutoka katika gari la polisi huku akimpeleka mtoni kunywa maji.

Aliyemuona aliwaita wanakijiji ambao bila kusita walifika kwa makumi chini ya dakika chache kabla ya kuanza kumpakulia polisi huyo adhabu.

Walimpata polisi huyo akiosha gari hilo ili kuodnoa chembechembe za kinyesi ambacho mnyama huyo alikuwa amejisaidia kwenye gari hilo.

Polisi huyo alinusuriwa baadae na kupelekwa katika kituo cha polisi