Baba mkwe agundua kijana anayemuoa bintiye ana sura mbaya, ataka harusi kusitishwa

Baba Mkwe alifika kwenye ukumbi wa kuandaa hafla ya harusi na pindi alipomuona kijana aliyetarajiwa kuwa mkwe wake, alitaka harusi hiyo kusimamishwa kwa kusema sura ya kijana huyo haikumpendeza.

Muhtasari

• Unahisi ni sahihi kwa mtu, haswa mrembo kuzingatia jinsi mpenzi wake anavyoonekana kabla ya kuingia katika ndoa naye?

Kuvunjika kwa uume kunaweza kutokea kwa sababu ya kubadilisha mitindo ya kujamiana wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Kuvunjika kwa uume kunaweza kutokea kwa sababu ya kubadilisha mitindo ya kujamiana wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Image: BBC NEWS

Harusi moja ililazimika kustishwa ghafla baada ya baba mkwe kudaiwa kutoa agizo hilo alipogundua kwamba kijana aliyepanga kufunga harusi na binti yake ana sura mbaya.

Kwa mujibu taarifa hiyo iliyogeuka kuwa mada ya mjadala katika kituo kimoja nchini Tanzania, babamkwe huyo ambaye hakutambuliwa kwa jina alifika katika siku kubwa ya binti yake lakini inaarifiwa baada ya kumuona mkwe mtarajiwa, hakupendezwa na sura yake.

Hapo ndipo mzee alijongea nyuma na kuwataka waandalizi wa hafla ya harusi kuipiga breki mara moja akisema kwamba hakuipenda sura ya bwana harusi ambaye alikuwa mkwe wake mtarajiwa.

Tukio hilo lisilo la kawaida lilizua mvutano mkali wa mawazo kutoka kwa watangazaji na watu waliochangia mada yenyewe.

Baadhi ya wanawake walisema kuwa sura au muonekano wa mwanaume wa kuzaa naye inazingatiwa sana, kando na elimu na utajiri ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikichukuliwa kama kigezo muhimu cha mwanamke anapomchagua mwanamume wa kuolewa naye.

Kwa upande wa wanaume, wengi walionekana kuchoshwa na vigezo vingi ambavyo wanawake wanawawekea kutoka utajiri, umbo la iraba minne, urefu, rangi ya ngozi ya hudhurungi na sasa sura pia.

Wengine pia walimsuta baba mkwe kwa kuingilia kati suala la mapenzi ya bintiye, kwani tayari alikuwa ameshamubali mkaka wa watu na sura hiyo ambayo baba aliikataa kuwa haina mshiko.

“Cha kwanza kwa mwanamume ni Amani, nafsi inasema nini kwako, ndio maana unaweza kupita barabarani ukamuona mtu kilema, kipofu au upungufu Fulani lakini ana mtu. Kwa mwanaume kinachokuwa na maana Zaidi ni Amani wala si sura. Mpaka anakupeleka kukutambulisha kwao mana yake ameshakubali kwamba hapa ndio tulizo langu la Amani liko,” mmoja alisema.

“Wanawake wakati mwingine wanataka vitu vingi sana, kuna muda watahitaji gym mtu wa miraba minne, kuna muda wanahitaji mtu wa ndevu, kuna muda wanahitaji mtu mrefu, mtu mwenye pesa,” mwingine alisema.

Unahisi ni sahihi kwa mtu, haswa mrembo kuzingatia jinsi mpenzi wake anavyoonekana kabla ya kuingia katika ndoa naye?