Wanandoa wamtesa njaa binti yao (5) karibia kufa baada ya pasta kusema ni mtoto mchawi

Kwa upande wao wazazi walisema kuwa wao hawakuhusika na njaa ya binti huyo kwa sababu walikuwa wakiishia hapo kutii tu unabii wa mchungaji wao kwamba mwanao ni ''mchawi,' hivyo ''hastahili kuishi.'

Muhtasari

• Mamake alisema pia alimfanya msichana huyo alale kwenye ubao kutokana na kujikojolea mara kwa mara na kukojoa mwilini mwake.

• Alidai kuwa msichana huyo wa miaka 5 alikuwa ‘’aliwajibika’ kwa kushindwa kwa mumewe.

Mtoto aliyeteswa njaa.
Mtoto aliyeteswa njaa.
Image: screengrab

Wanandoa nchini Nigeria wametiwa mbaroni baada ya kugundulika kumtesa mwanao wa miaka 5 njaa hadi karibia kufa baada ya kusemekana kwamba mchungaji wa kanisa lao aliwaambia mtoto huyo ni mchawi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, tukio hilio liliripotiwa katika jimbo la Anambra ambapo Kamishna wa Jimbo la Wanawake na Ustawi wa Jamii, Mhe. Ify Obinabo, alifichua haya katika taarifa mnamo Alhamisi, Septemba 7, 2023, alisema wazazi wa mwathiriwa walidai kuwa pasta alimwita mtoto huyo mchawi.

Akiwahutubia wahalifu katika afisi yake huko Awka, Mhe Obinabo alibainisha kuwa kazi yake ya msingi ni kulinda haki za kila mtoto jimboni iwe kutoka kwa serikali au la, na kuwahakikishia kwamba hatawaacha wahalifu waende huru.

Kwa upande wao watuhumiwa hao Bw.Michael Wosu (47) na Bi Blessing Michael (23) wa Akwa Ibom walisema kuwa wao hawakuhusika na njaa ya binti huyo kwa sababu walikuwa wakiishia hapo kutii tu unabii wa mchungaji wao kwamba mwanao ni ''mchawi,' hivyo ''hastahili kuishi.'

Blessing alisema pia alimfanya msichana huyo alale kwenye ubao kutokana na kujikojolea mara kwa mara na kukojoa mwilini mwake.

Alidai kuwa msichana huyo wa miaka 5 alikuwa ‘’aliwajibika’ kwa kushindwa kwa mumewe. Wakati huo huo, Michael Wosu alikanusha kuwa na habari kuhusu unyanyasaji aliofanyiwa mtoto huyo.

Kufikia wakati wa kuwasilisha ripoti hii, washukiwa bado wako chini ya ulinzi wa polisi huku manusura akipokea matibabu katika hospitali isiyojulikana huko Awka.