- Omondi alishtakiwa katika mahakama za Milimani siku ya Ijumaa pamoja na washirika wake kumi na watano kuhusu mkusanyiko usio halali na ulaghai nje ya bunge mnamo Februari 24, 2023.
Mcheshi Eric Omondi ameeleza kuwa yuko tayari kutumikia kifungo cha mwezi mmoja baada ya kufikishwa mahakamani.
Omondi alishtakiwa katika mahakama za Milimani siku ya Ijumaa pamoja na washirika wake kumi na watano kuhusu mkusanyiko usio halali na ulaghai nje ya bunge mnamo Februari 24, 2023.
Akijibu hukumu yake, mcheshi huyo alitumia akaunti yake ya Instagram ambapo alishiriki video yake na washukiwa kumi na watano wakiingia vyumbani. Alisema yuko tayari kutumikia kifungo cha mwezi mmoja kwani alikuwa na matumaini kwamba wangeshinda siku zijazo.
“Kwa hiyo leo mahakama imenihukumu mimi na vijana hawa kifungo cha mwezi mmoja jela. Tumehukumiwa kwa kupambana na gharama kubwa ya maisha. Inashangaza pia kwamba serikali iliongeza bei ya mafuta jana na haya ya ajabu yaliendana na tarehe yetu ya mahakama ambayo ni kwa ajili ya mapambano yale yale tuliyohukumiwa. Niko tayari kutumikia mwezi huo mmoja. Najua kesho tutakuwa washindi.” mcheshi alitangaza
Hii ni baada ya kesi iliyowasilishwa mahakamani ya kuwashitaki kwa kufanya maandamano nje ya bunge la kitaifa kuskilizwa na kusomwa na Jaji Lukas Onyina , wa mahakama ya hakimu Milimani hapa mjini Nairobi, Septemba 15.
Eric na wenzake, walikiri mbele ya Jaji wa mahakama ya hakimu ya milimani kuwa na hatia.
Polisi walidai kuwa bunge la kitaifa ni jumba ambalo hujiususha na mjadala wa mambo yanahuyu Taifa na hivy halitakiwi kuwa na usumbufu wowote.
Eric kwa upande wake, alidai walikua na lengo la kumuona Spika wa bunge ili kumkabidhi malalamishi na maslahi ya wakenga ambao alieleza kuwa wanakumbwa na hali ngumu ya maisha.
Hata hivyo Eric amekuwa akijishirikisha kwa shughuli ambazo kwa madai yake ni za kuwatetea Wakenya ambao anasema wameshindwa kukabiliana na hali ngumu ya maisha.