Ndoa nikuvumiliana-Mike Sonko awashauri wanandoa

Gavana huyo wa zamani wa Nairobi alisema kwamba unyanyasaji wa nyumbani una nafasi katika jamii ya kisasa.

Muhtasari
  • Sonko alianza kwa kushughulikia ongezeko la visa ambapo waume na wake wanakumbwa na mizozo kuhusu masuala madogo.
  • Alisisitiza umuhimu wa watu binafsi, hasa vijana wa kiume na wa kike wanaopanga kufunga ndoa, kuzingatia chaguo lao la wenzi wa ndoa.
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter alishiriki mawazo yake kuhusu hali ya ndoa za kisasa, hasa kutokana na video iliyosambazwa kwa kasi iliyohusishwa na Raymond Ndunga.

Gavana huyo wa zamani wa Nairobi alisema kwamba unyanyasaji wa nyumbani una nafasi katika jamii ya kisasa.

"Men at times some of us huwa na umbwakni sana kwani hamjui siku hizi mabibi hawapigwi," alishiriki na kuendelea kuangazia umuhimu wa kuchagua mwenzi wa maisha kwa busara na kukuza utangamano ndani ya ndoa.

Sonko alianza kwa kushughulikia ongezeko la visa ambapo waume na wake wanakumbwa na mizozo kuhusu masuala madogo.

Alisisitiza umuhimu wa watu binafsi, hasa vijana wa kiume na wa kike wanaopanga kufunga ndoa, kuzingatia chaguo lao la wenzi wa ndoa.

“Ndoa nikuvumiliana, maswala haya ya nyumbani hazitakangi hasira na mdomo” – Ndoa ni kuvumiliana, na masuala haya ya nyumbani yasiendeshwe kwa hasira na mabishano.

Alishiriki hadithi ya kibinafsi, akitoa shukrani kwa mkewe, Primrose Mbuvi, kwa usaidizi wake usioyumbayumba na uelewa wake wakati wa changamoto na furaha.

Mwanasiasa huyo mwenye shauku anaamini kwamba ufunguo wa kuendelea kwa ndoa au uhusiano wowote unategemea kuheshimiana na kusaidiana kati ya wenzi. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wenye uwiano, ambapo wenzi wote wawili huinuana badala ya kushindana au kudharauliana.

"Wakati mke wako atakapokuwa chini na kinyume chake, mukiishi hivyo ndoa yenu italast kwa miaka mingi," alisema.

Ushauri wa kutoka moyoni wa Mike Sonko umewagusa wengi kwenye mitandao ya kijamii, na kuzua mjadala kuhusu umuhimu wa kudumisha uhusiano wenye afya na wa kudumu.