Uchumi ni mbaya: Mama mboga amdunga kisu puani ng'ombe aliyevizia biashara yake

Inaarifiwa ng'ombe huyo sawa na tu na mifugo wengi wanaoonekana wakizurura katika maeneo ya masoko bila weneywe alikuwa akisaka chakula kabla ya kuvizia kwenye genge la mama mboga.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa toleo la Taifa Leo, kitendo hicho kilichohusishwa na hasira kutoka kwa mfanyibiashara huyo lilitokea majira ya jioni mnamo Oktoba 31.

Ng'ombe
Ng'ombe
Image: BBC NEWS

Kisa cha kutatanisha kilishuhudiwa katika soko la Kitengela kaunti ya Kajiado baada ya mama mfanyibiashara mdogo wa mboga za majani kumdunga kisu puani ng’ombe aliyekuwa anazengua karibu na genge lake la mboga.

Kwa mujibu wa toleo la Taifa Leo, kitendo hicho kilichohusishwa na hasira kutoka kwa mfanyibiashara huyo lilitokea majira ya jioni mnamo Oktoba 31.

Kulingana na picha zilizopigwa na kusambazwa mitandaoni, ng’ombe huyo anaonekana akitembea kando kando ya barabara akiwa na uchungu huku kisu hicho kikiwa bado kimekwama usoni karibu na pua lake.

Huku baadhi ya wakazi wakitaka shirika la ulinzi na matunzo kwa wanyama (KSPCA) kufuatilia tukio hilo na kumwokoa ng’ombe huyo, baadhi walitaka mwanamke huyo atiwe mbaroni mara moja kwa kitendo hicho cha kikatili, Taifa Leo walieleza.

Wengi wanakisia kwamba huenda mwanamke huyo alitenda kitendo hicho kwa kukerwa na mifugo ambao mara nyingi huonekana wakizurura katika maeneo ya masoko pasi na wenyewe.

Mama Mboga alitekeleza ukatili huo pasi na kupenda kwani uchumi umekuwa mbaya kiasi kwamba watu wamepatwa na msongo wa mawazo wengine hadi kufikia hatua za kufanya mambo kama hayo pasi na kupenda kwao.