Makanika auza magari 2 ili kuhamia Kanada, ajenti aishia kumpeleka Ivory Coast (video)

Fundi huyo alijikusanya kwa kila senti lake hadi kuuza magari yake mawili ili kupata kiasi cha pesa ambazo ajenti alimpa - zaidi ya dola za Kimarekani 3000 [Sh 457,800].

Muhtasari

• Alipofika Ivory Coast, alipata mshtuko wa maisha yake baada ya kugundua kuwa rafiki yake alikuwa amemlaghai.

• Kijana huyo fundi mitambo sasa amerejea katika taifa lake – Ghana - na anasimulia hadithi yake kama njia ya kuwaonya watu kuhusu ulaghai huu wa usafiri.

Jamaa aliyetapeliwa na ajenti.
Jamaa aliyetapeliwa na ajenti.
Image: TikTok//Screegrab

Fundi wa magari kutoka taifa la Ghana amechukua kwenye mitandao ya kijamii kuonesha kukerwa kwake na ajenti aliyemtapeli kiasi kikubwa cha pesa kwa ahadi ya kumpeleka nchini Kanada kutafuta unafuu kimaisha.

Fundi alieleza kwamba aliona ajenti huyo wa kusafirisha watu kwenda mataifa ya nje kikazi akitangaza huduma hizo kwenye mtandao wa Facebook.

Baadae aliwasiliana naye na wakaafikiana kiasi cha pesa ambazo angehitaji kuwa nazo ili kumudu mahitaji yote hadi kutua Kanada.

Fundi huyo alijikusanya kwa kila senti lake hadi kuuza magari yake mawili ili kupata kiasi cha pesa ambazo ajenti alimpa - zaidi ya dola za Kimarekani 3000 [Sh 457,800].

Mwisho wa siku, ajenti alimvusha tu mpaka na kumuingiza nchi jirani ya Ivory Coast, wakati makanika alikuwa na ndoto ya kufika Kanada na labda kubadilisha maisha yake.

Alipofika Ivory Coast, alipata mshtuko wa maisha yake baada ya kugundua kuwa rafiki yake alikuwa amemlaghai.

“Nilipofika huko [Ivory Coast], rafiki yangu aliyedai kuwa Kanada alinitembelea baada ya kwenda kwenye mahojiano hayo Ivory Coast, alikiri kuwa kuna fursa ya biashara nchini na kunitaka nijiunge nayo, nilihuzunika sana na kumwambia rafiki yangu kwamba udanganyifu wake ulikuwa umeniathiri vibaya."

Kijana huyo fundi mitambo sasa amerejea katika taifa lake – Ghana - na anasimulia hadithi yake kama njia ya kuwaonya watu kuhusu ulaghai huu wa usafiri.