logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kijana aliyeshikwa na vazi la polisi adai alilipata katika eneo la kuuza muguka Naivasha (video)

Alieleza kwamba koti hilo alifidiwa na jamaa anayeuza muguka ambaye alikuwa na redio yake.

image
na Davis Ojiambo

Habari27 March 2024 - 06:36

Muhtasari


  • • Hata hivyo, alikanusha kutumia koti hilo la polisi kutekeleza visa vya uhalifu akijifanya kuwa afisa wa polisi.
Kijana ashikwa na nguo za polisi.

Vijana wawili katika kaunti ndogo ya Molo kaunti ya Nakuru wametiwa mbaroni baada ya kukamatwa wakijifanya maafisa wa polisi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa video iliyonaswa na Citizen, vijana hao, mmoja alipatikana amevalia koti ya polisi na katika maelezo yake baada ya udadisi, alikiri kwamba koti hilo alilipata katika eneo la kuuzia muguka.

Alieleza kwamba koti hilo alifidiwa na jamaa anayeuza muguka ambaye alikuwa na redio yake na akamwambia kwamba haliwezi leta shida kwani si sare rasmi ya polisi.

“Hii jacket nilipata kwa shangazi yangu nilipoenda mazishi Naivasha, hapo ndio nilitokelezea hapo town kwa muguka. Kijana mwenye anauza muguka, nilikuwa na home theatre yangu akaniambia nipee hiyo woofer tubadilishane na jacket. Nikamuuliza haiwezi kuwa na shida, akaniambia ikiwa na kitambaa cha ndani haiwezi leta shida,” kijana huyo alielezea.

Hata hivyo, alikanusha kutumia koti hilo la polisi kutekeleza visa vya uhalifu akijifanya kuwa afisa wa polisi.

Tazama video hiyo hapa chini;

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved