Ex wa Jill Biden amkosoa kwa kumsukuma Joe Biden kusalia kwenye kinyang’anyiro cha urais

Joe Biden amepokea shinikizo kutoka kwa Wademokrati wakimtaka kujing'atua katika kinyang'anyiro hicho baada ya kudhalilishwa vibaya na mshindani wake Donald Trump katika mdahalo wa urais Alhamisi wiki jana.

Muhtasari

• Stevenson, 75, wa Delaware, ni mfuasi kindakindaki wa Trump ambaye amekuwa akiongea kwa miaka mingi juu ya uchungu wake na kile alichokiita "familia ya uhalifu ya Biden."

 

JOE NA JILL BIDEN.
JOE NA JILL BIDEN.

Mume wa zamani wa mama taifa wa Marekani,  Jill Biden amejiunga na kikundi cha watu wanaomkashifu kwa kumshinikiza Rais Biden abaki kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa urais, baada ya kufanya vibaya katika mdahalo wa kwanza wa urais Alhamisi iliyopita.

"Dk. Jill Biden ambaye nimemuona kwenye TV katika miaka mitano iliyopita sio mtu yule yule niliyefunga naye ndoa au ninayemtambua kwa njia yoyote," Bill Stevenson, ambaye alioana na Jill kutoka 1970 hadi 1975, aliiambia jarida la The Post Jumamosi.

"Amesomeshwa na kuwa mwanamke tofauti kabisa."

Stevenson, 75, wa Delaware, ni mfuasi kindakindaki wa Trump ambaye amekuwa akiongea kwa miaka mingi juu ya uchungu wake na kile alichokiita "familia ya uhalifu ya Biden."

"Sielewi kwa nini anashikilia sana kumtetea na kumweka kwenye kinyang'anyiro kwani inaonekana anajitahidi," Stevenson alisema.

"Inaonekana kuwa anapambana na kila mtu siku hizi. Nimemwona Jill akikua," aliongeza.

"Nimekuwa nikijivunia kwake wakati fulani. Sina hisia kali ... nashangaa tu kumuona mbele na katikati ya vita hivi baada ya kuruka chini ya rada kwa miaka mingi. Daima amekuwa akiendeshwa sana. Watu wanasema yeye ndiye anataka kuwa rais sasa."

Stevenson, ambaye alioa tena na ana familia yake mwenyewe, aliwahi kumuunga mkono Biden, alipogombea kama makamu wa rais na Barack Obama na wakati Biden alipogombea Seneti ya Merika mnamo 1972.