logo

NOW ON AIR

Listen in Live

MP wa Kimilili Didmus Barasa ajitangaza kama mwenyekiti wa Gen Z

Makataa ya kuwasilishwa kwa majina kutoka vikundi mbalimbali ni Julai 7.

image
na Davis Ojiambo

Habari01 July 2024 - 05:51

Muhtasari


  • •   Hata hivyo, wengi walimkumbusha kwamba Gen Z hawana uongozi na wala hawana haja ya kujigawanya kwa misingi ya ukabila.
DIDMUS BARASA

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa amejiteua na kujitangaza kama mwenyekiti wa vuguvugu la vijana wa Gen Z.

Kupitia ukurasa wake wa X, Barasa alisema kwamba aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya vijana hao kuonekana kutokuwa na kiongozi na hata kusisitiza kwamba hawana haja ya kuwa na uongozi ili matakwa yao kusikilizwa.

Barasa alisema kwamba yeyote atakayejaribu kupinga hilo atatembelewa na vijana kwa ‘salamu’ ambayo ni kutafuta namba yake na kuiweka bayana mitandaoni kwa watu umpigia simu na kumtumia jumbe.

Pia mbunge huyo wa UDA alitangaza kuwa yuko mbioni kumtafuta makamu wake.

“Leo nimejiteua kuwa mwenyekiti wa Gen Z. Sasa nahitaji Makamu mwenyekiti....kuanzia sasa Gen Z wasiseme hawana kiongozi tena. Mwenye anasena ngoooo...tunaenda kumusalimia ile salamu yetu,” Barasa aliandika.

Hata hivyo, wengi walimkumbusha kwamba Gen Z hawana uongozi na wala hawana haja ya kujigawanya kwa misingi ya ukabila.

Tangazo la Barasa linakuja siku mbili baada ya rais Ruto kuomba Gen Z kuwasilisha majina ya wawakilishi 2 wa jinsia yoyote kwa kamati itakayoundwa kushughulikia masuala ibuka nchini.

Makataa ya kuwasilishwa kwa majina kutoka vikundi mbalimbali ni Julai 7.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved