Waititu asema Ruto ana mambo 2 ya kufanya baada ya maandamano ya Gen Z

Kulingana naye, kuwafuta kazi washirika wake ndiyo njia pekee ambayo watu watarejesha matumaini kwake.

Muhtasari
  • Kulingana naye, kuwafuta kazi washirika wake ndiyo njia pekee ambayo watu watarejesha matumaini kwake.
Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu
Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu
Image: MAKTABA

Aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu amemshauri rais aidha kujiuzulu au kuwafuta kazi makatibu wake wote wa baraza la mawaziri, na uongozi wa juu kuhusiana na hadhi ya taifa kwa sasa.

Kulingana naye, kuwafuta kazi washirika wake ndiyo njia pekee ambayo watu watarejesha matumaini kwake.

Waititu aliendelea na kueleza kuwa kinachoendelea si cha kipekee nchini Kenya, kilitokea Misri na Tunisia, na kusababisha kujiuzulu kwa viongozi wao.

“Kinachotokea si cha Kenya pekee, kilitokea Misri na Tunisia na kusababisha kujiuzulu kwa viongozi wao. Suluhu pekee alilonalo rais ni kujiuzulu au kuwafuta kazi makatibu wake wote wa baraza la mawaziri na uongozi ili watu warudishe matumaini kwake,” alisema.

Rais wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali alikimbilia Saudi Arabia tarehe 14 Januari 2011 kufuatia maandamano ya Mapinduzi ya Tunisia. Rais wa Misri Hosni Mubarak alijiuzulu tarehe 11 Februari 2011 baada ya siku 18 za maandamano makubwa, na kumaliza miaka 30 ya urais wake.

Vijana wa Kenya wamekuwa wakipanga kwenye mitandao ya kijamii maandamano ya amani mitaani yaliyokusudiwa kulazimisha mamlaka kufuta mswada wa fedha wa 2024. Maandamano hayo yalianza Juni 18 baada ya mswada huo kuwekwa hadharani kwa mara ya kwanza.