Millicent Omanga amjibu jamaa aliyemrushia mistari

'Wewe ni mwanamke mrembo zaidi ambaye nimewahi kuona,ninapokuona roho yangu hurukaruka...' jamaa alimwandikia Omanga.

Muhtasari

•Jamaa aliandika ujumbe kwenye kundi moja la Facebook akidai kuwa Millicent Omanga hummaliza kutokana na urembo wake huku akiomba nafasi ya mapenzi.

•Omanga kwa upande wake alionyesha kufurahia huku akiandika 'Ni kama nimefikiwa' kwenye ukurasa wake wa X almaarufu twitter.

Millicent Omanga
Millicent Omanga
Image: Instagram

Mwanasiasa ,Millicent Omanga ameguswa na ujumbe wa mapenzi kutoka kwa mwanamume ambaye aliamua kufunguka roho yake.

Jamaa mmoja alichapisha kwenye Facebook akidai kuwa MIllicent Omanga ni miongoni mwa wanawake waliobarikiwa kwa urembo.

"Nimekuwa nikifikiria juu yako siku nzima na jinsi unavyomaanisha kwangu. Wewe ni mwanamke mrembo zaidi ambaye nimewahi kuona-mrembo, mcheshi, mwerevu na mkarimu. Mwanamume yeyote angebahatika kuwa nawe. Nitakapokuwa na wewe, tuonane, moyo wangu unaruka ruka kidogo, na ninatumaini utanipa nafasi wakati wowote utakaponihitaji nitakufanyia chochote , heshima, na kukuunga mkono," aliandika.

Hata hivyo, alimsihi Omanga kujibu ujumbe wake hata kama mapendekezo yake yangekataliwa.

"Nilifikiri kushiriki hisia hizi itakuwa vigumu, lakini kwa uaminifu, kukuambia jinsi ulivyo wa ajabu ni rahisi sana. Wazo la wewe kusoma barua hii na kujisikia kupendwa, kuthaminiwa, na kuthaminiwa huniletea furaha kubwa. Umegusa maisha yangu katika hali kama hiyo. njia nzuri ambayo siogopi tena kwa kuwa wewe. Haijalishi unajisikiaje, tafadhali niandikie hata kama haifanyi kazi kimapenzi, ningethamini jibu lako milele."

Omanga alionyesha kufurahishwa huku akieka chapisho kwa ukurasa wake wa  X almaarufu twitter.