Hisia mseto baada ya Didmus Barasa kuhudhuria mazishi ya kijana aliyepigwa risasi wakati wa uvamizi wa bunge

Marehemu aliuawa kwa kupigwa risasi wakati waandamanaji walipovamia majengo ya bunge mwishoni mwa mwezi uliopita.

Muhtasari

•Barasa alikuwa miongoni mwa mamia ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya marehemu Willy Sitati katika eneo la Kimilili, kaunti ya Bungoma.

•"Shauku yake na kujitolea kwake kwa kazi hiyo haitasahaulika, na kumbukumbu yake itatutia moyo kuendelea kujitahidi kwa maisha bora ya baadaye," Barasa alisema.

katika mazishi ya Willy Sitati
Mbunge Didmus Barasa katika mazishi ya Willy Sitati
Image: X// DIDMUS BARASA

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameeleza hisia mseto baada ya Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa kujitokeza kwenye maziko ya mwathiriwa wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha ambayo yalishuhudia idadi kubwa ya vijana wakiuawa kwa kupigwa risasi.

Barasa alikuwa miongoni mwa mamia ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya marehemu Willy Sitati katika eneo la Kimilili, kaunti ya Bungoma mnamo Jumamosi. Marehemu alidaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi wakati waandamanaji walipovamia majengo ya bunge mwishoni mwa mwezi uliopita.

Katika taarifa yake aliyoichapisha kwenye  mtandao wa Twitter baada ya mazishi hayo, Mbunge huyo wa UDA ambaye ni miongoni mwa wanasiasa waliokosolewa sana wakati wa maandamano hayo alisherehekea maisha ya marehemu Willy na azma yake katika kupigania haki.

"Leo, tulimzika Willy Sitati, mwanachama kijana wa Generation Z ambaye maisha yake yalikatizwa kwa huzuni wakati wa uvamizi wa Bunge hivi majuzi. Kifo cha ghafla cha Willy kinatumika kama ukumbusho wa kuhuzunisha wa umuhimu mkubwa katika kupigania haki na mabadiliko,” Barasa alisema Jumamosi.

Aliongeza, "Shauku yake na kujitolea kwake kwa kazi hiyo haitasahaulika, na kumbukumbu yake itatutia moyo kuendelea kujitahidi kwa maisha bora ya baadaye. Pumzika kwa amani Willy.”

Mbunge huyo aliambatanisha taarifa yake na picha zake akiwa miongoni mwa waombolezaji wengine wakati wa maziko yaliyofanyika katika eneo bunge analowakilisha.

Akizungumza katika hafla hiyo, alitoa wito kwa mamlaka kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha aliyempiga risasi Willy anakamatwa na kuadhibiwa.

"Polisi wanapaswa kuchana kila jiwe. Fanya uchunguzi ufaao kupata mtu ambaye alihusika na kifo cha Willy cha ghafla,” alisema.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii hata hivyo wamejibu kwa hisia mseto huku wachache wakimpongeza kwa uwepo wake katika mazishi hayo, wengine wakimkosoa huku wengine wakimsukuma kudai haki.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya kwenye X:

Japeth Ekidor-Doyen: You should condemn the regime for being rogue as well. Killing protestors wasn’t good.

Isaac Babu: Kimilili, you guys are cheering a MP who supported a bill that resulted in loss of lives. Mtaumiaumia kiasi. I don’t think you have suffered enough.

Sunukei2024: Was expecting a paragraph in your statement to talk about justice for the life lost. The officer who shot him should face the law.

Dickson Ochora: A traitor should not appear in these events.

Wycliffe Wangwe Wekesa: May his soul Rest in Peace.