logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kalonzo:Raila alilazimika kubadilisha nambari ya simu baada ya Gen Z 'kumsalimia'

Kalonzo aelezea sababu ya Raila Odinga kubadilisha nambari yake ya simu.

image
na Davis Ojiambo

Habari11 July 2024 - 12:02

Muhtasari


  • •Kalonzo alisema kuwa ilibidi Raila Odinga kubadilisha nambari ya simu kwa kuwa ilisambazwa mtandaoni na alipokea jumbe nyingi zikimlazimisha kutafuta nambari mbadala. 
  • •Makamu huyo wa zamani wa rais aliwataka wakenya kukoma kumdhulumu Raila mitandaoni na kuwataka wawe wakarimu kwa 'baba'

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amefichua kuwa kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga amelazimika kubadilisha nambari yake ya simu.

Akizungumza siku ya Alhamisi, Julai 11 katika kongamano la Vijana la Pan African, Kalonzo alisema kuwa nambari ya simu ya waziri mkuu huyo wa zamani ilisambazwa mtandaoni na alipokea jumbe nyingi zikimlazimisha kutafuta nambari mbadala.

“Nilizungumza naye (Raila) nikiwa njiani kuja hapa…. watu walienda kumtembelea jana ikabidi abadilishe namba yake ya simu kwa sababu Gen Z waliweka namba kila mahali,” alisema Kalonzo.

Makamu huyo wa zamani wa rais aliwataka wakenya kukoma kumdhulumu Raila mitandaoni na kumfanyia wema.

"Labda ni kipimo cha uonevu wa mtandaoni tafadhali kuweni wakarimu kwa baba. Iwapo wanaweza kufanya hivyo kwa Raila Odinga, fikiria nani mwingine katika nchi hii hatafanyiwa hivo” Kalonzo aliongeza.

Raila amekuwa akishutumiwa tangu Jumanne, Julai 9 baada ya kukaribisha kuundwa kwa kongamano la sekta mbalimbali kushughulikia masuala yaliyoibuliwa na Gen Z wakati wa maandamano ya hivi majuzi.

Hata hivyo jambo hilo halikuwapendeza vijana wa Gen Z wakidai kuwa wao hawana kiongozi na hawamtambuwi yeyote kama kiongozi wao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved