logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbunge Farah afukuzwa kwenye hoteli kufutia 'kauli yake dhidi ya vijana waandamanaji'

Bw. Kariuki asisitiza kuwa hoteli hiyo haikubaliani kwa vyovyote na kauli ya Maalim.

image

Habari13 July 2024 - 09:30

Muhtasari


  • Katika video iliyosambaa kwa kasi mitandaoni mbunge huyo anaonekana akisema ‘’waandanaji walifanya uhaina na laita angelikuwa rais angeliwaua’’
Farah Maalim, mbinge wa Daadab

Mbunge wa Dadaab Farah Maalim amefukuzwa katika hoteli moja mjini Mombasa pwani ya Kenya kufuatia kauli yenye utata aliyotoa hivi karibuni dhidi ya waandamanaji vijana wa Gen Z.

Katika video iliyosambaa kwa kasi mitandaoni mbunge huyo anaonekana akisema ‘’waandanaji walifanya uhaina na laita angelikuwa rais angeliwaua’’

Vyombo vya Habari vya ndani vinaripoti kuwa Mbunge huyoalifika katika hoteli hiyo siku ya Ijumaa.

Mkurugenzi Mkuu wa hoteli hiyo Jimi Kariuki alitoa tangazo la kufukuzwa kwa mbunge huyo katika mtandao wa X zamani Twitter baada ya baadhi ya watumiaji wake kuishtuma kwa kumruhusu kukaa hapo.

Bw. Kariuki asisitiza kuwa hoteli hiyo haikubaliani kwa vyovyote na kauli ya Maalim.

Katika video hiyo ambayo haijulikani ilirekodiwa lini, Maalim, akizungumza kwa lugha ya Kisomali anaonekana, akisema kuwa kama angekuwa Rais wa Kenya angewaua waandamanaji 5,000 kila siku.

Tafsiri ya video iliyothibitishwa ilifichua kuwa mbunge huyo alikuwa akiwashutumu Vijana wa Kenya kwa jaribio lao la kuandamana hadi Ikulu wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa fedha wa 2024.

Mbunge huyo hata hivyo amekanusha madai hayo akisema video hiyo ilifanyiwa ukarabati.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved